Serikali
imesema leo kuwa mawaziri wakuu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM)
wataendelea kulipwa pensheni zao kwa mujibu wa sheria ya nchi.
Mawaziri
wakuu hao; Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga
na Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema)na badaye Lowassa aligombea
urais chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).




Mtu mmoja Jijini Mbeya (PICHANI JUU) ambaye hakuweza kutambulika kwa
Majina,inadaiwa amekutwa amefariki leo asubuhi kwenye moja ya uchochoro wa nyumba zilizopo katika mtaa wa Mwamfupe.