TANGAZO

TANGAZO
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo THOMAS WIKESI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo THOMAS WIKESI. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 3 Agosti 2016

Tazama video maonesho ya nane nane mkoani ,morogoro yakiendelea huku Wananchi wa Tanzania waombwa kutumia hasa bidhaa zinazo tengeneza hapa nchini.



Wafanyabiashara na wakulima nchini wametakiwa kupenda bidha zinazozalishwa ndani ya nchi badala yake wasipendelee kutumia bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa mauzo kutoka Kampuni ya Old Ease International JOHN MCHARO mapema hii leo wakati akiongea na WIKESI BLOGS kwenye Maonesho ya Nane nane katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere mkoani Morogoro.

Jumamosi, 2 Aprili 2016

TASWIRA 11, NEWCASTLE YA BENITEZ IKIPIGWA 3-2 NA NORWICH, SASA IMECHUNGULIA DARAJA LA KWANZA



Leo, Newcastle imechapwa mabao 3-2 dhidi ya Norwich. Kama ikiruhusu ifungwe tena mechi ijayo, basi itakuwa imeteremka daraja ikiwa chini ya Kocha Rafa Benitez ambaye amejiunga nayo ili awe mkombozi.

Jumanne, 22 Machi 2016

Man City kuanza zama za Guardiola kwa kusajili wachezaji wanne au watano wenye majina makubwa

Man City kuanza zama za Guardiola kwa kusajili wachezaji wanne au watano wenye majina makubwaViongozi wa City wanaamini mazingira mazuri ya kazi, na nguvu ya usajili vitamshawishi meneja wao mpya kudumu klabuni zaidi ya miaka mitatu
Manchester City watampa Pep Guardiola ushirikiano kwa asilimia mia moja katika mkakati wa kuunda kikosi imara kwa kusajili wachezaji wanne au watano wenye majina makubwa majira ya joto,

Inaaminika kuwa simu za mkononi za Guardiola na Mkurugenzi wa michezo wa City Txiki Begiristain zimekuwa zikipokea simu nyingi kutoka kwa mawakala wa wachezaji wenye uwezo mkubwa kutoka Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Bundesliga na kwingineko.

Conte akanusha vikali tetesi za kibarua cha Chelsea


Conte akanusha vikali tetesi za kibarua cha Chelsea
Kocha huyo wa Italia amehusishwa vikali na tetesi za kutua Darajani Stamford lakini yeye amesisitiza kuwa akili yake yote ipo pamoja na Azzurri kuelekea Euro 2016
Kocha huyo wa Italia Bw. Antonio Conte amekanusha taarifa hizo zinazodai kuwa anakaribia kuwa meneja wa Chelsea, akisisitiza kuwa akili yake ipo kwenye kibarua chake cha timu ya taifa inayojiandaa na michuano ya Euro 2016.

Jumatatu, 21 Machi 2016

MKUU WA WILAYA NJOMBE SARA DUMBA AFARIKI DUNIA


Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa ya kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe na aliewahi kuwa Mtangazaji wa Radio Tanzania RTD, alievuma sana na kipindi cha Mama na Mwana na vipindi vingine vingi, Dada Sara Dumba, kilichotokea ghafla usiku huu.

Jumatano, 10 Februari 2016

Kiasi Cha Fedha Atakachokuwa Akilipwa Mourinho Man Utd Na Muda Wa Mkataba Wake Watajwa

Tetesi za kupewa kwa Jose Mourinho na klabu ya Manchester United zinazidi kushika hatamu kila dakika.
 
Gazeti la kila siku El Confidencial leo limeripoti taarifa za ndani za mkataba unaosubiriwa kusainiwa baina ya Jose Mourinho na waajiri wake wapya Manchester United.
Taarifa za ‘Special One’ kubeba mikoba ya Van Gaal zimechapishwa na kila chombo cha habari huko England asubuhi ya leo.
Vichwa vya habari vya magazeti vimeandika kwamba: Jose Mourinho amewaambia marafiki wa karibu kwamba atakuwa boss mpya wa United kuanzia msimu ujao.

FC BARCELONA WATINGA FAINALI KWA KISHINDO BAADA YA KUWEKA REKODI HII...................

Sare ya bao 1-1 iliyoipata FC Barcelona dhidi ya Valencia jana usiku katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Copa del Rey siyo kwamba imeiwezesha kutinga fainali ya michuano hiyo pekee bali pia imeiwezesha miamba hiyo ya Catalunya kuweka rekodi ya kucheza michezo 29 bila kupoteza mchezo hata mmoja katika michuano yote na kuvunja rekodi yake ya mwaka 2010/11 ya kucheza michezo 28 bila kupoteza.

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo February 11 2016 kwenye Udaku, Hardnews na michezo


February 11 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea mtu wangu..

TUTARAJIE MABADILIKO HAYA KATIKA KOMBE LA MABINGWA BARANI ULAYA UEFA..............


Vilabu vikubwa barani ulaya vinajadili mbinu za kufanyia marekebisho ligi kuu ya mabingwa barani humo.
Vilabu hivyo hata hivyo vimepuzilia mbali uvumi kuwa wanapendekeza kuvunjwa kwa ligi hiyo na kuanzishwa kwa ligi mbadala ya 'Super League'.

Muungano wa vilabu barani humo European Clubs' Association (ECA) linasema kuwalinapanga kufanya marekebisho hayo kwa ushirikiano na UEFA ifikapo mwaka wa 2018.

Azam FC kuzialika Tanzania TP Mazembe, Zesco United


COVER

Habari na mtandao wa AzamFC:
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kuwa mwenyeji wa michuano maalumu ya kimataifa ya timu nne itakayofanyika mwanzoni mwa mwakani.
Michuano hiyo ni ile waliyoenda kushiriki jijini Ndola Zambia hivi karibuni na kutwaa ubingwa, ambapo imeanzishwa kwa muungano wa klabu tatu, Azam FC, TP Mazembe na Zesco United.

Jumapili, 7 Februari 2016

ANGALIA PICHA KIBAO ZA USHAHIDI JINSI ZOUMA ALIVYOUMIA JANA KWENYE GEMU DHIDI YA MAN UNITED.. GET WELL SOON......


Beki wa kati wa Chelsea, Kurt Zouma ameumia goti lake upande wa nyuma baada ya kutua vibaya wakati akirejea chini alipokuwa akiwania mpira wa juu katika mechi dhidi ya Man United iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.

Ijumaa, 5 Februari 2016

UNAJUA KINACHOMUWEKA BENCHI MAGURI? MWENYEKITI WA STAND ATUMBUA JIPU

Elius Maguri, Mshambuliaji wa Stand United anatesa baada ya kutemwa MsimbaziElius Maguri, amejikuta akichezea mkeka ndani ya kikosi cha Stand United licha ya kuwa kwenye kiwango bora kwa sasa
Mshambuliaji wa Stand United Elius Maguli siku za hivi karibuni amekuwa haonekani dimbani kutokana na kuchezea mkeka ndani ya kikosi cha Stand United chini ya kocha mfaransa Patrick Liewig.

STORY MPYA KUHUSU CHANONGO NA UBWA NDANI YA TP MAZEMBE

ddKimya kimetanda tangu wachezaji wa Stand United Haruna Chanongo na Hassan Ubwa walipokwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DR na hatimaye kurejea nchini kimyakimya bila klabu ya Stand kuwajulisha watanzania majibu ya wachezaji hao kama wamefuzu au wamekwama.

Hii hapa namba ya waliokamatwa kwa kuchoma mali za watuhumiwa wa mauji ya Diwani Muleba Kagera…(+Audio)


Ripoti kutokea Mkoa wa Kagera kuhusu lile tukio la mauaji ya Diwani aliyevamiwa na watu usiku akitazama Habari nyumbani kwake, Wananchi waliamua kuchoma mali za watuhumiwa wa mauaji, Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi, Augustine Ollomi kwenye sentensi zake; – RPC Augustine Ollomi
Ni kweli kuna watu 13 tunawashikiria wanawake watatu na wanaume 10 kwa tuhuma za kuharibu mali za watuhumiwa wa mauaji kwa madai walihusika na mauaji ya Diwani wa Kata ya Kimwani Wilaya ya Muleba Kagera, Syliveste Mulinga ( CUF ), ;- RPC Ollomi

BABA WA NEYMAR AFICHUA DAU LILILOTENGWA NA MAN UTD KWA AJILI YA MWANAE

Neymar-in-court
Baba mzazi wa mchezaji wa Barcelona, Neymar Jr wiki hii amefichua siri juu pesa ya ambayo klabu ya Manchester United waliyoitenga msimu uliopita kutaka kumsajili mtoto wake kutoka Barcelona,  huku wakiwa tayari kukidhi buyout clause iliyowekwa na Barcelona ya pauni 145m ili kumnasa mbrazili huyo.
Neymar Snr ambaye amemsindikiza mwanae katika kesi inayowakabili ya kutoweka wazi kiasi sahihi cha pesa ambayo FC Barcelona walitoa kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Santos ya Brazil, amesema kuwa Manchester United walitenga mezani mamilioni hayo ya fedha kumtaka mwanae lakini akasisitiza kuwa hajui kitakachotokea mbeleni,  ila bado kijana wake ana mkataba wa misimu 2 na ana furaha  Nou Camp.

Alhamisi, 4 Februari 2016

INASIKITISHA… Jamaa kaota mizizi kwenye mwili wake


Moja ya ripoti iliyonifikia kutokea nchini Bangladesh ni hii ya jamaa kuugua ugonjwa wa kuota mizizi katika sehemu za viungo vyake vya mwili.
Abul Bajandar  alianza kupata hali miaka 10  iliyopita, ugonjwa huu unajulikana kama epidermodysplasia verruciformi au “ugonjwa wa binadamu mti”.
Serikali ya Bangladesh kupitia kwa Waziri wa afya Mohammad Nasim imesema itagharimia upasuaji wa kijana huyo.

MESSI AWEKA REKODI NYINGINE KWENYE MAISHA YAKE YA SOKA

Messi-500

 Messi ameandika rekodi nyingine tena kwenye maisha yake ya soka wakati FC Barcelona ikiiangushia kipondo ‘heavy’ timu ya Valencia kwenye mchezo wa kombe la mfamle Hispania maarufu kama Copa del Rey.

VPL: SIMBA MWENDO MDUNDO, YANGA YACHECHEMEA, MATOKEO, MSIMAMO NA WAFUNGAJI YAPO HAPA

SIMBA SC imejiweka sawa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga Mgambo JKT mabao 5-1 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
http://1.bp.blogspot.com/-mYophk0enlc/VjG3Q2q8iOI/AAAAAAAAq2I/2JFGgKDo1Kw/s640/VPL-logo.jpg
Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 39 baada ya kucheza mechi 17, sasa ikiwa inazidiwa pointi moja tu na mabingwa watetezi, Yanga SC walio kileleni, wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 39 pia.

Jumatano, 3 Februari 2016

Baba yake Neymar kataja kuwa imemfikia ofa ya pound milioni 144.4 kwa ajili ya Neymar, The Sun wataja klabu inayomtaka


Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar, bado yupo kwenye headlines kuhusiana na suala lake la usajili kutoka Santos kujiunga FC Barcelona mwaka 2013, kudaiwa kuwa na magumashi kiasi cha yeye kufikishwa mahakamani kutoa ushahidi.

Jumatano, 27 Januari 2016

‘Lowassa, Sumaye watandelea kupata pensheni’



Edward Lowassa na Fredrick Sumaye 
Serikali imesema leo kuwa mawaziri wakuu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM) wataendelea kulipwa pensheni zao kwa mujibu wa sheria ya nchi.
Mawaziri wakuu hao; Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema)na badaye Lowassa aligombea urais chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).