TANGAZO

TANGAZO

Jumatatu, 6 Julai 2015

Video ikionyesha walichokifanya Abdu Kiba na Ruby nyuma ya Camera!

Abdu 1Ni dakika chache ambazo zinakutangulizia kuona kitachofata kwenye video mpya ya Abdu Kiba ft. Ruby (Ayaya) ambayo ni single mpya kwenye radio kwa wiki kadhaa sasa hivi.
Location ya hii video ni White Sand Dar es salaam Tanzania.

KUTAZAMA VIDEO HII BOFYA

KESHI ATUPIWA VIRAGO NIGERIA

KeshiShirikisho la Soka nchini Nigeria limetangaza kumsitishia ajira ya kuinoa timu ya Taifa ya Nigeria ‘The Super Eagles’ kocha Steven Keshi.

Siku saba za urais ndani ya CCM


Dar/Dodoma. Ni wiki ngumu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM). Ndivyo unavyoweza kusema kwani chama hicho kinachotawala kitafanya vikao vyake vya juu vitakavyohitimishwa kwa kumpata mgombea wake wa urais.

Kikwete: Msimchague huyu




Tanga. Rais Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa dini nchini kuwahimiza waumini wao kuwachagua wanasiasa wasiokuwa waovu, wasiofanana na uovu au hata kuukaribia.
Amewataka kuepuka makundi ya kisiasa na wasiwape mwanya wanasiasa wenye dhamira ovu katika kutafuta madaraka kwa thamani yoyote na wawakemee wale wanaotaka kupata madaraka kwa gharama yoyote.

Mbunge ajivua uanachama Chadema


Sumbawanga. Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi ametangaza kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akizungumza mjini Mpanda katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, jana Arfi aliwaeleza wananchi wa Mpanda kuwa uanachama wake ndani ya Chadema utakoma mara tu baada ya kuvunjwa Bunge Julai 9.

Ijumaa, 3 Julai 2015

Upinzani ‘walianzisha’ tena bungeni




Dodoma. Mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika jana ulizua kizaazaa na kumlazimisha Spika Anne Makinda kuahirisha kikao baada ya kukosekana utulivu ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Kikao hicho kiliahirishwa muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu wakati Bunge lilipotakiwa kukaa kama kamati kumalizia kiporo cha Muswada wa Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi wa mwaka 2015 ambao mchakato wa kuupitisha haukukamilika juzi kutokana na muda kuisha.

Alhamisi, 2 Julai 2015

Rick Ross ni jela au mtaani? Haya hapa kutoka Mahakamani na video yake..

       Rick-Ross-court


Headlines za Entertainment Marekani zilikuwa na story ya Rick Ross kukamatwa na kuwekwa ndani yeye pamoja na bodyguard wake, kesi yao ilikuwa ni ishu ya kuteka na kujeruhi watu wawili.
July 01 2015 kapandishwa Mahakamani, Georgia Marekani.. Kesi ikasomwa na milango ikawa wazi kwa jamaa kuwekewa dhamana