TANGAZO

TANGAZO

Ijumaa, 5 Februari 2016

STORY MPYA KUHUSU CHANONGO NA UBWA NDANI YA TP MAZEMBE

ddKimya kimetanda tangu wachezaji wa Stand United Haruna Chanongo na Hassan Ubwa walipokwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DR na hatimaye kurejea nchini kimyakimya bila klabu ya Stand kuwajulisha watanzania majibu ya wachezaji hao kama wamefuzu au wamekwama.

Hii hapa namba ya waliokamatwa kwa kuchoma mali za watuhumiwa wa mauji ya Diwani Muleba Kagera…(+Audio)


Ripoti kutokea Mkoa wa Kagera kuhusu lile tukio la mauaji ya Diwani aliyevamiwa na watu usiku akitazama Habari nyumbani kwake, Wananchi waliamua kuchoma mali za watuhumiwa wa mauaji, Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi, Augustine Ollomi kwenye sentensi zake; – RPC Augustine Ollomi
Ni kweli kuna watu 13 tunawashikiria wanawake watatu na wanaume 10 kwa tuhuma za kuharibu mali za watuhumiwa wa mauaji kwa madai walihusika na mauaji ya Diwani wa Kata ya Kimwani Wilaya ya Muleba Kagera, Syliveste Mulinga ( CUF ), ;- RPC Ollomi

BABA WA NEYMAR AFICHUA DAU LILILOTENGWA NA MAN UTD KWA AJILI YA MWANAE

Neymar-in-court
Baba mzazi wa mchezaji wa Barcelona, Neymar Jr wiki hii amefichua siri juu pesa ya ambayo klabu ya Manchester United waliyoitenga msimu uliopita kutaka kumsajili mtoto wake kutoka Barcelona,  huku wakiwa tayari kukidhi buyout clause iliyowekwa na Barcelona ya pauni 145m ili kumnasa mbrazili huyo.
Neymar Snr ambaye amemsindikiza mwanae katika kesi inayowakabili ya kutoweka wazi kiasi sahihi cha pesa ambayo FC Barcelona walitoa kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Santos ya Brazil, amesema kuwa Manchester United walitenga mezani mamilioni hayo ya fedha kumtaka mwanae lakini akasisitiza kuwa hajui kitakachotokea mbeleni,  ila bado kijana wake ana mkataba wa misimu 2 na ana furaha  Nou Camp.

Alhamisi, 4 Februari 2016

INASIKITISHA… Jamaa kaota mizizi kwenye mwili wake


Moja ya ripoti iliyonifikia kutokea nchini Bangladesh ni hii ya jamaa kuugua ugonjwa wa kuota mizizi katika sehemu za viungo vyake vya mwili.
Abul Bajandar  alianza kupata hali miaka 10  iliyopita, ugonjwa huu unajulikana kama epidermodysplasia verruciformi au “ugonjwa wa binadamu mti”.
Serikali ya Bangladesh kupitia kwa Waziri wa afya Mohammad Nasim imesema itagharimia upasuaji wa kijana huyo.

MESSI AWEKA REKODI NYINGINE KWENYE MAISHA YAKE YA SOKA

Messi-500

 Messi ameandika rekodi nyingine tena kwenye maisha yake ya soka wakati FC Barcelona ikiiangushia kipondo ‘heavy’ timu ya Valencia kwenye mchezo wa kombe la mfamle Hispania maarufu kama Copa del Rey.

VPL: SIMBA MWENDO MDUNDO, YANGA YACHECHEMEA, MATOKEO, MSIMAMO NA WAFUNGAJI YAPO HAPA

SIMBA SC imejiweka sawa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga Mgambo JKT mabao 5-1 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
http://1.bp.blogspot.com/-mYophk0enlc/VjG3Q2q8iOI/AAAAAAAAq2I/2JFGgKDo1Kw/s640/VPL-logo.jpg
Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 39 baada ya kucheza mechi 17, sasa ikiwa inazidiwa pointi moja tu na mabingwa watetezi, Yanga SC walio kileleni, wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 39 pia.

Jumatano, 3 Februari 2016

Baba yake Neymar kataja kuwa imemfikia ofa ya pound milioni 144.4 kwa ajili ya Neymar, The Sun wataja klabu inayomtaka


Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar, bado yupo kwenye headlines kuhusiana na suala lake la usajili kutoka Santos kujiunga FC Barcelona mwaka 2013, kudaiwa kuwa na magumashi kiasi cha yeye kufikishwa mahakamani kutoa ushahidi.