Wafanyabiashara na wakulima nchini wametakiwa kupenda bidha
zinazozalishwa ndani ya nchi badala yake wasipendelee kutumia bidhaa
zinazozalishwa nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa mauzo kutoka Kampuni
ya Old Ease International JOHN MCHARO mapema hii leo wakati akiongea na WIKESI
BLOGS kwenye Maonesho ya Nane nane katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere
mkoani Morogoro.
Kampuni hiyo inayohusika na kuzalisha vifaa mbalimbali vya
Mashine za printer ndiyo ya kwanza
hapa nchini Tanzania kuwa na kiwanda kinachozalisha bidhaa hiyo Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla.
Hata hivyo Mcharo amesema kuwa Maonesho ya Nane nane yanayonedelea katika viwanja hivyo vya Mwalimu Nyerere Mkoani
Morogoro, yanafaa kutokana na wakulima wanapata elimu mbalimbali ikiwemo mbinu
za kilimo cha kisasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni