TANGAZO

TANGAZO

Ijumaa, 5 Februari 2016

STORY MPYA KUHUSU CHANONGO NA UBWA NDANI YA TP MAZEMBE

ddKimya kimetanda tangu wachezaji wa Stand United Haruna Chanongo na Hassan Ubwa walipokwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DR na hatimaye kurejea nchini kimyakimya bila klabu ya Stand kuwajulisha watanzania majibu ya wachezaji hao kama wamefuzu au wamekwama.


Mwenyekiti wa Stand United ya mjini Shinyanga. amesema mchakato wa Chanongo na Ubwa ulmeingia figisu japo ripoti kutoka Mazembe zinasema wamefuzu majaribio yao.

“Taarifa zilizopo ni kweli kwamba wale mabwana kwenye ile interview ya kwanza Chanongo alikuwa amefuzu lakini Ubwa alipewa nafasi nyingine lakini naye pia nafikiri alifuzu. Lakini kuna vitu ambavyo vilikuwa vinaendelea kati yetu sisi na TP Mazembe na hata wachezaji walivyotoka kule waliambiwa wasubiri Dar es Salaam ili wawape majibu ya kujiunga nao”, Amani Vicent.

“Kwahiyo na wao waliondoka wakiwa wametoa taarifa kwa uongozi lakini kocha akawa hakupewa taarifa za kutosha lakini nafikiri kuna jambo liliingia katikati kwasababu kipindi wanaondoka kwenda Mazembe tayari kulikuwa na suala la uongozi kurudishiwa simu na wale ambao walikuwepo walikuwa wanafikiri kama ingewezekana kufanyika biashara kwenye mikono yao”.

“Kwahiyo nafikiri kuna figisu ndogo ziliingia ambazo zinaleta madhara mwisho wa siku wata-join kwenye klabu na ni wachezaji wetu wana mkataba bado tunawahitaji japokuwa hilo lilimkwaza kocha, ni mambo ya kawaida ambayo yanaweza kutokea kwenye michezo. Tulizingatia zaidi mafanikio ya wachezaji kuliko kufikiria maslahi ya mtu mmojammoja”.

Chanongo na Ubwa wapo nchini lakini muda wote wapo jijini Dar es Salaam tangu waliporejea majuma kadhaa kutoka nchini Congo DR walikokwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya TP Mazembe huku klabu yao ya Stand ikiendelea kukosa huduma yao.
chanzo:shafii dauda

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni