TANGAZO

TANGAZO

Jumapili, 7 Februari 2016

MATOKEO YA GEMU ZOTE ZA VPL LEO, YANGA, SIMBA, AZAM ZASHINDA, ANGALIA SASA MSIMAMO ULIVYO

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/09/vpla-426x360.jpgMshambuliaji wa yanga Saimon Msuva hii leo ameiongoza timu yake kuibuka na ushindi wa goli 4-0 mbele ya JKT Ruvu yeye akifunga goli 2 katika ushindi huo mnono, unaowaweka kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya vodacom kwa pointi 1 zaidi ya Simba SC na Azam FC.

Katika mchezo huo yanga sc walienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0, zilizofungwa na Saimon Msuva katika dakika ya 12 na Issoufou Bobackari katika dakika ya 43 ya mchezo


Yanga SC walianza mchezo kwa kasi na kuonyesha dhamira ya kutaka kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo lakini ilibidi wangoje mpaka dakika ya 12 goli la Saimon Msuva kuwapa uongozi huo.

Kuingia kwa goli hilo kuliwaimarisha JKT Ruvu lakini yanga SC walikuwa na kasi zaidi pale wanapo saka goli katika mchezo huo wa leo ambapo walienda mapumziko wakiwa mbel kwa goli 2-0.

Katika kipind cha pili Yanga SC waliendeleza kasi yao ya kusaka goli huku JKT Ruvu wakitolea na kutafuta goli taratibu,

Katika dakika ya 62 Donald Ngoma aliiandikia Yanga SAC goli la 3 kabla ya Saimon Msuva kuhitimisha katika dakika 3 za nyongeza na kupelekea mchezo kumalizika kwa yanga sc kuibuka na ushindi wa goli 4-0,

Kwa matokeo hayo Yanga SC wamefikisha pointi 43, wakibakia katika usukani wa ligi wakifuatiwa kwa karibu na Simba SC na Azam FC wenye pointi 42 kila mmoja


Kule Kagera

Katika uwanja wa Kambarage Simba SC walikuwa wageni wa Kagera sugar ambao walikuwa hawajapoteza mchezo toka wahamie katika uwanja huo wa CCM Kambarage wakitokea katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Tabora. 

Katika mchezo huo goli la Simba SC lilifungwa na Ibrahim Ajibu katika kipindi cha kwanza huu, na kuipeleka Simba Sc mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha pili Simba SC waliapata penati ambayo Ibrahim Ajibu alikosa penati hiyo, ikiwa ni kabla ya mchezaji wa Kagera sugar kuzawadiwa kadi nyekundu katika dakika ya 80 ya mchezo na kupeleka mchezo kumalzika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Kiujumla Simba SC walipoteza nafasi kadha za kufunga magoli huku wakitawala mchezo katika vipindi vyote viwlili vya mchezo.

Katika uwanja wa Azam Complex, Azam FC wao walikuwa wenyeji wa Mwadui FC na mchezo huo ulimalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililo fungwa na Kipre Herman Tcheche.

Katika mchezo huo Mwadui FC hawakuwa na bahati, walitengeneza nafasi nyingi za wazi lakini walishindwa kuzitumia na kupelekea ushindi ubakie hapo Chamanzi.


Kutoka Songea
Vijana wa kocha Bakari Shime Mgambo Shooting hali imeendelea kuwa mbaya kwao baada ya leo kukubali kichapo cha goli moja bila toka kwa majimaji FC, mchezo uliochezwa mjini Songea
Kichap hicho cha goli 1-0 toka kwa Majimaji FC ni muendelezo wa matokeo mabovu waliyokuwa wanayapata katika siku za karibuni ambapo katika michezo 4 wameambulia pointi 1 pekee.

Wakati Mgambo shooting wakikbulai kichapo jirani zao Coastal union nao wamekubali kichapo cha goli 2-1 toka kwa Coastal union, ikiwa ni muendelezo wa jinamizi la kuifunga yanga sc.

Coastal union toka waifunge yanga sc wamecheza michezo miwili ambapo wamepoteza yote hiyo.



MATOKEO YA MICHEZO YA LEO KWA UJUMLA

MBEYA CITY 0-0 TANZANIA PRISONS
 
MAJIMAJI 1-0 MGAMBO JKT
 
NDANDA FC 1-1 MTIBWA SUGAR
 
AZAM FC 1-0 MWADUI FC
 
YANGA SC 4-0 JKT RUVU
 
TOTO AFRICAN 2-1 COASTAL UNION
 
KAGERA SUGAR 0-1 SIMBA SC

BAADA YA MICHEZO YA LEO MSIMAMO UKO HIVI 

RnTimuPWDLFAGdPts
1YANGA1813414293343
2SIMBA SC18133233102342
3Azam FC16133031102142
4MTIBWA SUGAR189632112933
5STAND UNITED179261713429
6T. PRISONS178541817129
7MWADUI FC188461916328
8TOTO AFRICANS174671521-618
9MBEYA CITY174581522-717
10MGAMBO SHOOTING174581522-717
11NDANDA FC173771518-316
12KAGERA SUGAR184311921-1215
13Coastal Union172781118-713
14JKT RUVU1834111729-1213
15AFRICAN SPORT183411519-1413
16MAJIMAJI FC1734101031-2113

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni