Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil
anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar, bado yupo kwenye
headlines kuhusiana na suala lake la usajili kutoka Santos kujiunga FC
Barcelona mwaka 2013, kudaiwa kuwa na magumashi kiasi cha yeye
kufikishwa mahakamani kutoa ushahidi.
Moja kati ya stori zilizotumika kupamba
headlines za gazeti la The Sun, ni stori kuhusu Neymar kuhusishwa
kujiunga na klabu ya Man United ya Uingereza ambayao imetaja kutenga dau
la uhamisho wa kihistoria katika soka la pound milioni 144.4.
Stori za Neymar kuhitajika kwa dau la
pound milioni 144.4 inaripotiwa kutolewa na baba yake mzazi, ambaye
anasema kuwa tayari amepokea ofa ya pound milioni 144.4 kutoka kwa moja
ya vilabu vya Ulaya lakini sio hakutja jina la klabu na kuongezea kuwa
sio Real Madrid klabu hiyo, uchunguzi wa The Sun unatajwa kufanikiwa
kujua jina la klabu ambayo inatajwa kuwa ni Man United.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni