Serikali
imesema leo kuwa mawaziri wakuu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM)
wataendelea kulipwa pensheni zao kwa mujibu wa sheria ya nchi.
Mawaziri
wakuu hao; Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga
na Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema)na badaye Lowassa aligombea
urais chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Akijibu
maswali ya baadhi ya wabunge waliohoji endapo watu waliokuwa katika
nyadhifa hizo wanaweza kuzuiwa kuchukua pensheni zao kwa kuhamia
upinzani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma, Angellah
Kairuki amesema sheria haizuii kwa kuwa kuhama chama ni haki ya
kikatiba.
Akinukuu
Sheria ya mwaka 1999 pamoja na ile ya mwaka 2005 ya Utumishi wa Umma,
Kairuki amesema waliokuwa viongozi katika nyadhifa hizo wana haki ya
kuendelea kupata stahiki hizo kisheria.
Hata hivyo ameonya kuwa, wanapaswa kuheshimu sheria ya nchi inayowazuia kutoa siri za nchi wakati wakiwa katika nyadhifa zao.
Kwa
upande mwingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji,
amesema uchumi ukiimarika utaisaidia serikali kuwalipa wastaafu pensheni
itakayokidhi mahitaji yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni