Mtu mmoja Jijini Mbeya (PICHANI JUU) ambaye hakuweza kutambulika kwa
Majina,inadaiwa amekutwa amefariki leo asubuhi kwenye moja ya uchochoro wa nyumba zilizopo katika mtaa wa Mwamfupe.
Kifo
cha Mtu huyo ambaye inaelezwa ni kijana wa makamo alikutwa amefariki
kwenye uchochoro wa nymba hiyo mara baada ya kubainika na baadhi ya
Wananchi,waliokuwa wakikatiza mtaa huo kuelekea mtaa mwingine,Baadhi ya
Mashudhua wa eneo hilo wameeleza kuwa mtu huyo si mkazi wa mtaa huo,
"Mtu
huyo si Mkazi wa Eneo hili, bali Jioni ya jana waliomuona maeneno hayo
akiwa katika hali ya
kupepesuka Pepesuka kotokana na kunywa Pombe, na huenda hicho ndicho
kilicho pelekea Kifo chake kwani hakuwa mwenye afya njema." Alibainisha
mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo wakati akihojiwa na Mwandishi wa Globu
ya Jamii iliofika eneo la tukio
Baadhi ya Wanachi wa Mtaa wa Mwamfupe wakijadiliana jambo
katika eneo la tukio.
Huzuni ikatawa Eneo hilo.
Baadhi
ya Wanachi sambamba na Wenyenyumba zilizo zunguka Eneo hilo la
Tukio wakisubiri msaada kutoka Jeshi la Polisi.Globu ya Jamii
inafuatilia taarifa kamili kutoka kwa jeshi la Polisi mkoani Mbeya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni