Moshi.
Jeshi la Polisi limefanikiwa kumtia mbaroni mkazi mmoja wa jijini Dar
es Salaam, anayetuhumiwa kujifanya mganga wa kienyeji na kumtapeli mke
wa mmiliki wa shule moja ya sekondari Sh600 milioni.
Mtuhumiwa
huyo alifanikiwa kutapeli fedha hizo baada ya mwanamke huyo kukataa
ushauri wa awali kuwa ili dawa ya kufanya wanafunzi wafurike shuleni
hapo ifanye kazi, waue mwanafunzi mmoja kimazingara. Alipokataa ushauri
huo ndipo alipoambiwa atoe fedha ili atengenezewe dawa mbadala.
“Yuko
hapo kituo kikuu cha Mkoa wa Kilimanjaro. Mimi nilimuuliza ilikuwaje
akasema ni kweli alichukua fedha hizo lakini kwa makubaliano ya uganga.
Inaonekana kuna zaidi ya uganga,” alidokeza polisi mmoja.
Kamanda
wa polisi wa mkoa, Ramadhan Mungi aliomba apewe muda hadi leo
atakapotoa taarifa sahihi, lakini wiki iliyopita aliyekuwa kaimu kamanda
wa mkoa, Koka Moita alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.
chanzo:mwananchi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni