PICHA:NA MAKTABA
NA THOMAS WIKESI
WAZIRI wa nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Sera,Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu,Mheshimiwa
Jenista Mhagama amewataka watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro
kuacha kufanya kazi kwa mazoea endapo wanahitaji kuendelea kuwepo kazini.
Mheshimiwa Mhagama ametoa kauli hiyo hii
leo mjini Morogoro katika aliyoifanya ya kukagua shughuli mbalimbali
zinazofanywa na vijana ambapo ametoa muda wa siku saba kwa uongozi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuwatafutia vijana maeneo maalumu ya
kufanyia shughuli za kuzalisha mali.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya
Morogoro,Pasco Kihanga licha ya kukiri kuwepo kwa mapungufu katika utendaji
kazi kwa baadhi yaa watumishi wa Manispaa hiyo ameiombaa Serikali kuhakikisha
inawapatia vijana elimu ya biashara kabla ya kuwapatia fedha za mikopo kwa
ajili ya kujiendeleza kiuchumi tofauti na ilivyo sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni