Kahama. Wakati
serikali ikipigia kelele kukemea imani za kishirikina, wilayani Kahama
bado ni kitendawili baada ya mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwamande, Kata ya
Mwanase katika Halmashauri ya Msalala kufariki na baadaye wanakijiji
kumzika na mali zake zote yakiwemo makreti ya bia na soda aliyokuwa
akiyatumia kwenye biashara yake ya baa.
Tukio
hilo limetokea jana katika kijiji hicho baada ya mwanakijiji huyo,
Mahushi Lutaja kufariki na baadaye familia yake kupitisha maadhimio ya
kumzika na mali zake zote kwa imani ya kwamba kifo chake kimetokana na
kurogwa na wao kuhofia kwamba wakibaki na mali zake nao watakumbwa na
mauti.
Kwa
mujibu wa diwani wa Kata ya Mwanase, Samson Masanja, Lutaja baada ya
kifo chake alizikwa na baisikeli moja vitanda vinne na magodolo yake
pamoja na masanduku ya nguo zake zote na vitu vingine vidogovidogo
alivyokuwa akivitumia
Pia
Masanja alisema, Lutaja alizikwa na makreti ya bia na soda ambayo kabla
ya kifo chake alikuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya kuuza vinywaji
kwenye kijiji hicho cha Mwamande ambapo tukio hilo limehusishwa na
imani za kishirikina
Wakati
akiugua ndugu zake waliamini kwamba ugonjwa huo uliopelekea kifo chake
ulitokana na kurogwa hivyo familia yake iliingiwa na hofu hiyo hasa
kutokana na kuwepo madai ya waganga wa jadi kuamini kwamba ndugu yao
alirogwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni