TANGAZO
Jumatatu, 4 Januari 2016
Kipindu pindu cha shika kasi Manspaa ya Morogoro
Afisa afya Manispaa ya Morogoro:GABRIEL MALISA
Picha :maktaba
Na Thomas Wikesi
Kutokana namilipuko wa Ugonjwa wa kipindupindu mkoani morogoro ,Afisa afya wa manispaa ya MOROGORO Bwana Gabriel Malisa amewataka wakazi wa manspaa ya hiyo kuwa makini na vyakula ambavyo wanakula hasa kwa mamantilie .
Akizungumza Na Thomas blog Malisa Amesema wameanza
mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo kama vile kufungia biashara za MAMA LISHE maarufu kama MAMA NITLIE ,Kuzuia biashara ya Matunda ya kumenywa pia kuzuia biashara ya pombe za kienyeji .
Wagonjwa wa kipindu pindu walianza kupokelewa katika kituo cha Afya cha Sabasaba ambapo ndipo wamewekewa kambi mnamo Tarehe 23 Mwezi wa 12 .
Dk.Sandra Baraka ambae ni daktari katika kambi hiyo ya wagonjwa wa Kipindu pindu amesema mpaka sasa wamepokea wagonjwa 59 tangu waanze kupokea wagonjwa hao 23 desember na watoto wakiwa 6 .pia wagonjwa wagonjwa wengine wameruhusiwa ila mpaka sasa kambi ina wagonjwa 24 .
Ameongeza kuwa kambi yao inajitahidi kwani ni ndogo ina uwezo wa kuchukua wagonjwa 16.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni