SABABU 5 KWANINI MESUT OZIL NI KIPAJI ADIMU
Tangu atue Arsenal misimu miwili iliyopita kwa ada ya pauni milioni
42 kutoka Real Madrid mchezaji Mesut Özil, klabu yake ya Arsenal imekua
hailali njaa.
Wametwaa makombe ya chama cha soka FA cup katika misimu hii miwili
mfululizo, Ozil akiwa chachu ya mafanikio hayo. Msimu huu pia Arsenal
wako kileleni hadi sasa na tayari Mesut Ozil anakaribia kuvunja rekodi
ya kutoa pasi nyingi za magoli (assists) hadi sasa ana assists 16, si
kitu cha kawaida.
Kuna kitu lazima ufikirie hivi pamoja na ubahiri wa kiasi hicho wa
kocha Arsene Wenger lakini alithubutu kutoa pesa nyingi kiasi hicho
pauni milioni 42. Hapa chini nimejaribu kuandika sababu zinazomfanya
kijana huyu raia wa Ujerumani kuwa ni kipaji cha kipekee kabisa katika
kikosi cha Arsenal na ligi kuu England kwa ujumla;
Umakini (awareness)
Unaweza kuyaangalia macho ya Mesut Ozil ukadhania unavyodhani wewe,
lakini kwangu mimi ananikumbusha Ronaldinho Gaucho ama Frank Lampard
walivyokua na jicho la kipekee kutazama wapi anaupeleka mpira kabla
haujamfika miguuni kwake. Ozil ni aina wachezaji wajanja-wajanja
wanapokua uwanjani kitu kinachomfanya awe bora zaidi katika eneo la tatu
la kiwanja.
Sio mbinafsi (selflessness)
Huwezi kuwa kinara wa kupiga pasi za mabao kwa wachezaji wenzako kama
wewe ni mchoyo. Mesut Ozil kama alivyokua Gaucho ni wachezaji wazuri
mno kwa pasi za mwisho na hufikiria zaidi kutoa pasi kuliko kufunga wao.
Msimu umefika katikati tayari Ozil amepiga assists 16 ni rekodi ya aina
yake.
‘Touch’ yake ya kwanza
Katika kitu ambacho mshambuliaji Robin Van Persie alikua anafaulu
sana anapopata mpira, basi ni ile touch yake ya kwanza ya mpira. Hapa
lazima uwe mwanahisabati kwelikweli, vinginevyo huwezi kuwa fundi na
utapoteza mipira mingi. Kwa Mesut Ozil touch yake ya kwanza ndio huwa
hatari zaidi kwani kutokana na umakini wake anakua tayari alishajua wapi
kwa kuupeleka huo mpira.
Mipira iliyokufa (free kick)
Tofauti na ilivyokua wakati Thierry Henry ama Robin Van Persie
wakipiga kona ama mipira mingine ya adhabu, Ozil amekua na mipira ya
adhabu yenye madhara zaidi kuliko waliomtangulia. Jaribu kuchunguza
mipira ya kona ya kijana huyu inapokua inazunguka kutoka katika eneo la
kona hadi golini, mara nyingi husababisha hatari zaidi kwa wapinzani.
Mwepesi
Wakati anatua Arsenal ilikua ni ngumu kuona kama angeweza kukidhi
misukosuko ya ligi kuu nchini England, ligi ambayo inasifika kwa
matumizi makubwa ya nguvu, kasi na pumzi ya kutosha. Lakini sanjari na
asili yake ya uvivu (casualness) katika muonekano wake inamfanya aweze
kuwa mwepesi na ‘threat’ katika eneo la tatu la kiwanja kwani ni rahisi
pia kuonekana kafanyiwa faulo kutokana na kutokua na ubavu kama walionao
akina Mulumbu na Check Tiote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni