Serikali
imepoteza jumla ya Sh48.47bilioni baada ya makontena 11,884 na magari
2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.
Hata
hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na
Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa
mapato.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ufisadi huo umebainika baada
ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini
Dar es Salaam.
Akifafanua,
Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh
47.4 bilioni wakati magari gari 2019 zenye thamani ya sh 1.07bilioni
yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa tozo.
chanzo:MWANANCHI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni