Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula
Dar
es Salaam. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Angelina Mabula amefanya ziara ya kushtukiza Ofisi za Baraza la Ardhi na
Nyumba za Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kukuta zaidi ya
nusu ya watendaji wake wako likizo.
Naibu
Waziri huyo aliwasili ofisini hapo jana saa 8.30 mchana na kupokewa na
mtunza kumbukumbu, Bahati Kassim ambaye ni mtumishi pekee aliyekuwapo
ofisini.
Baada ya kusaini kitabu cha wageni, naibu waziri aliuliza waliko watumishi wengine.
Naibu Waziri: Watumishi wengine wako wapi?
Bahati: Wako likizo na mmoja ametoka kikazi.
Naibu Waziri: Baraza lina watumishi wangapi hapa Kinondoni.
Bahati: Tupo watumishi sita.
Naibu Waziri: Wangapi wako likizo.
Bahati: Wanne, tumebaki wawili, mmoja ambaye ni mwenyekiti ametoka ana kazi za nje.
Baada
ya kujibiwa hivyo, Mabura alisema haiwezekani watumishi wanne wakawa
likizo kwa wakati mmoja, wakati baraza lina watumishi sita.
“Kuna mpangilio mbaya wa likizo, hii ina maana kuna siku ofisi zitafungwa kwa sababu watumishi mtakuwa likizo,” alisema.
Mtunza
kumbukumbu pia alimueleza kati ya mwaka 2004 hadi sasa, kuna kesi zaidi
ya 2,000 zilizofikishwa mbele ya baraza hilo na kati ya Januari hadi
sasa, wamepokea kesi 300.
Awali,
Mabula alitembelea kijiji cha King’azi kinachogombewa na wilaya za
Kisarawe na Kinondoni ambako aliunda timu ya wataalam watakaochunguza
mipaka ya vijiji vya King’azi, Msopwa na Mloganzila ili kubaini viko
upande gani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni