Shinyanga.
Serikali imesema madaktari wote watakaopata nafasi ya kusoma nje ya
nchi kwa ufadhili wake, watafanya hivyo kwa kusaini mkataba.
Kufanya hivyo kumeelezewa kuwa kutasaidia kuwabana wale wanaohitimu na kutimkia nje ya nchi kwenda kufanya kazi huko.
Hayo
yalisemwa na Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na
Watoto, Dk Hamis Kigwangalah alipotembelea Manispaa ya Shinyanga.
Alisema Serikali imeendelea kuwapoteza madaktari wengi inaowasomesha wanaokimbia kwa madai ya mazingira mabovu ya kufanyia kazi.
Wengi wao hukimbilia nchi za Afrika Kusini na Botswana wanakodai kuna mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
Alisema wanataka kuona wizara inakuwa na madaktari bingwa wa kutosha kulika ilivyo sasa.
Awali,
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, Fredrick Mlekwa
alimwambia naibu waziri huyo kuwa, tatizo kubwa linalokwamisha utendaji
kazi wao ni upungufu wa madaktari hospitali hapo.
Dk
Mlekwa alisema hospitali hiyo ina madaktari bingwa wanne, madaktari wa
kawaida 15 na madaktari wasaidizi kumi na moja. Alisema kwa mwaka hutoa
huduma kwa wagonjwa zaidi ya 500,000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni