TANGAZO

TANGAZO

Jumanne, 8 Desemba 2015

PLUIJM HATAKI MCHEZO, AMPIGA CHINI MDOGOAKE MSUVA

Simon Msuva akamlisha keki  mdogowake James Msuva (kulia) siku aliyokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa (birthday) December 3, 2015
Simon Msuva akamlisha keki mdogoake James Msuva (kulia) siku aliyokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa (birthday) December 3, 2015
Kama ulikua hujui sasa nakufanya ujue kuwa kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm hataki kabisa mchezo linapokuja suala la kazi, hii imemkuta kiungo wa timu hiyo James Msuva ambaye ni mdogo wa Simon Msuva baada ya kuachwa na kocha huyo wakati kikosi cha Yanga kikiingia kambini kujiandaa na mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

James Msuva amejikuta katika wakati mgumu siku chache baada ya kupandishwa kwenye kikosi cha kwanza aitokea kikosi B cha timu hiyo.
Siku chache zilizopita James Msuva alichelewa kufika mazoezini ambapo wakati anaripoti alikuta tayari wachezaji wengine walikuwa wameshaanza kufanya mazoezi, alipotaka kuungana na wachezaji wenzake katika mazoezi ghafla akajikuta ameingia katika wakati mgumu baada ya Van Pluijm kumchimba ‘mkwara’ mzito na kumwamuru akae pembeni kuwapisha wachezaji wengine waendelee na mazoezi.
Baada ya timu kumaliza mazoezi ya siku hiyo Van Pluijm alimwita James Msuva na kumwambia hatoingia kambini na kikosi cha Yanga na badala yake atabaki nyumbani hiyo ikiwa kama adhabu kwa kosa lake la kuchelewa mazoezini.
Timu ya ushindi ya shaffihdauda.co.tz ikamtafuta James Msuva ili kumuuliza kulikoni yeye na kibabu wa Yanga na hatma yake kwenye kikosi cha kwanza, ndipo mchezaji huyo akasema kocha mkuu wa Yanga (Van Pluijm) amemwambia apumzike kwanza kuma adhabu ya kuchelewa mazoezini na hatokuwa sehemu ya wachezaji watakaoingia kambini kujiandaa na mwendelezo wa mechi za ligi kuu zitakazoendelea December 12.
“Siku ileile niliyochelewa mazoezini aliniambia kwamba, Jumatatu timu inaingia mazoezini lakini mimi nisiende”, amesema kinda huyo ambaye ni mdogo wa nyota wa timu hiyo Simon Msuva.
“Nimeshamuomba msamaha amenisamehe lakini kikubwa alichosisitiza ni kwamba, nisiende kambini na nijifunze kitu”.
Kikosi cha Yanga tayari kimeingia kambini tangu Jumatatu December 7 kuanza kujiandaa na mechi zao za ligi kuu Tanzania bara ambapo wao wataanzia mkoani Tanga watakapocheza mechi mbili wakiwa huko.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni