Kocha
wa Mbeya City, Abdul Mingange amesema atatumia muda wa mapumziko
kujipanga upya kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.
Katika mechi ya mwisho, Mbeya Cuty ilipoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga.
“Huu muwa wa mapumziko ni mzuri kujipanga, tunaweza kuangalia mambo kadhaa tuliyokosea na kuangalia tufanye nini,” alisema.
Mingange alisema kikosi chao kimekuwa kikicheza soka safi lakini kuna mambo kadhaa kama umaliziaji analazimika kuyafanyia kazi.
chanzo:Saleh Jembe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni