TANGAZO

TANGAZO

Jumanne, 22 Desemba 2015

RAIS KAGAME AMPONGEZA MAGUFULI

Rais John Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura (kushoto) baada ya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam jana. Picha Ikulu Dar es Salaam. Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam na kumhakikishia kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ya usafirishaji. Rwanda, ambayo haijapakana na bahari, imekuwa ikiitegemea Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kupitisha zaidi ya asilimia 70 ya mizigo yake. Rais Kagame, ambaye miaka miwili ilkiyopita aliwahi kukosoa waziwazi utendaji wa Bandari akieleza kuwa angepewa taasisi hiyo angeweza kukusanya mapato ambayo yangeiendesha Tanzania, sasa anaonekana kuridhishwa na hatua za Serikali ya Awamu ya Tano za kudhibiti mianya ya kukwepa kodi, kuondoa uzembe na kupambana na ufisadi kwenye bandari hiyo kongwe. Akiwasilisha salamu za pongezi kwa Rais Magufuli baada ya kuchaguliwa kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura alieleza jinsi Rais Kagame alivyofurahishwa na hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya viongozi wa Bandari. Kwa upande wake, Rais Magufuli alimhakikishia Balozi Kayihura kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Rwanda ili wananchi wa nchi zote mbili waweze kunufaika kimaendeleo. Dk Magufuli alimuomba Kayihura kumfikishia Rais Kagame salamu za shukrani kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa Rais na kwamba amedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda. Mapema mwezi huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo kushughulikia matatizo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL). Pia, alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadh Massawe na kuagiza uchunguzi dhidi yao uanze mara moja, alivunja Bodi ya Wakurugenzi TPA. Kushirikiana na ADB Katika hatua nyingine, Rais amemhakikishia mwakilishi mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Dk Tonia Kandiero kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo ya kifedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Pamoja na kumhakikishia ushirikiano, Rais ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya kuelekea katika utekelezaji wa miradi na badala yake ameshauri uwepo utaratibu wa haraka unaowezesha kuanza kwa miradi katika kipindi kifupi baada ya fedha kutolewa. Kwa upande wake, Dk Kandiero alisema benki hiyo iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo kama ambavyo imekuwa ikifanya na kwamba kwa sasa imetenga Dola 2.3 bilioni kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Alisema ADB imelenga kujielekeza kutoa mikopo katika sekta ya nishati na usafiri.

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
            Rais John Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura (kushoto) baada ya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam jana. Picha Ikulu

Dar es Salaam. Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam na kumhakikishia kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ya usafirishaji.

Rwanda, ambayo haijapakana na bahari, imekuwa ikiitegemea Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kupitisha zaidi ya asilimia 70 ya mizigo yake.

Rais Kagame, ambaye miaka miwili ilkiyopita aliwahi kukosoa waziwazi utendaji wa Bandari akieleza kuwa angepewa taasisi hiyo angeweza kukusanya mapato ambayo yangeiendesha Tanzania, sasa anaonekana kuridhishwa na hatua za Serikali ya Awamu ya Tano za kudhibiti mianya ya kukwepa kodi, kuondoa uzembe na kupambana na ufisadi kwenye bandari hiyo kongwe.

Akiwasilisha salamu za pongezi kwa Rais Magufuli baada ya kuchaguliwa kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura alieleza jinsi Rais Kagame alivyofurahishwa na hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya viongozi wa Bandari.

Kwa upande wake, Rais Magufuli alimhakikishia Balozi Kayihura kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Rwanda ili wananchi wa nchi zote mbili waweze kunufaika kimaendeleo.

Dk Magufuli alimuomba Kayihura kumfikishia Rais Kagame salamu za shukrani kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa Rais na kwamba amedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda.

Mapema mwezi huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo kushughulikia matatizo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).

Pia, alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadh Massawe na kuagiza uchunguzi dhidi yao uanze mara moja, alivunja Bodi ya Wakurugenzi TPA.

Kushirikiana na ADB

Katika hatua nyingine, Rais amemhakikishia mwakilishi mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Dk Tonia Kandiero kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo ya kifedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Pamoja na kumhakikishia ushirikiano, Rais ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya kuelekea katika utekelezaji wa miradi na badala yake ameshauri uwepo utaratibu wa haraka unaowezesha kuanza kwa miradi katika kipindi kifupi baada ya fedha kutolewa.

Kwa upande wake, Dk Kandiero alisema benki hiyo iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo kama ambavyo imekuwa ikifanya na kwamba kwa sasa imetenga Dola 2.3 bilioni kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Alisema ADB imelenga kujielekeza kutoa mikopo katika sekta ya nishati na usafiri.

Rais John Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura (kushoto) baada ya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam jana. Picha Ikulu Dar es Salaam. Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam na kumhakikishia kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ya usafirishaji. Rwanda, ambayo haijapakana na bahari, imekuwa ikiitegemea Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kupitisha zaidi ya asilimia 70 ya mizigo yake. Rais Kagame, ambaye miaka miwili ilkiyopita aliwahi kukosoa waziwazi utendaji wa Bandari akieleza kuwa angepewa taasisi hiyo angeweza kukusanya mapato ambayo yangeiendesha Tanzania, sasa anaonekana kuridhishwa na hatua za Serikali ya Awamu ya Tano za kudhibiti mianya ya kukwepa kodi, kuondoa uzembe na kupambana na ufisadi kwenye bandari hiyo kongwe. Akiwasilisha salamu za pongezi kwa Rais Magufuli baada ya kuchaguliwa kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura alieleza jinsi Rais Kagame alivyofurahishwa na hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya viongozi wa Bandari. Kwa upande wake, Rais Magufuli alimhakikishia Balozi Kayihura kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Rwanda ili wananchi wa nchi zote mbili waweze kunufaika kimaendeleo. Dk Magufuli alimuomba Kayihura kumfikishia Rais Kagame salamu za shukrani kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa Rais na kwamba amedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda. Mapema mwezi huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo kushughulikia matatizo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL). Pia, alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadh Massawe na kuagiza uchunguzi dhidi yao uanze mara moja, alivunja Bodi ya Wakurugenzi TPA. Kushirikiana na ADB Katika hatua nyingine, Rais amemhakikishia mwakilishi mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Dk Tonia Kandiero kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo ya kifedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Pamoja na kumhakikishia ushirikiano, Rais ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya kuelekea katika utekelezaji wa miradi na badala yake ameshauri uwepo utaratibu wa haraka unaowezesha kuanza kwa miradi katika kipindi kifupi baada ya fedha kutolewa. Kwa upande wake, Dk Kandiero alisema benki hiyo iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo kama ambavyo imekuwa ikifanya na kwamba kwa sasa imetenga Dola 2.3 bilioni kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Alisema ADB imelenga kujielekeza kutoa mikopo katika sekta ya nishati na usafiri

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni