Wema Sepetu alizaliwa tarehe 28, September, ni mtoto wa mwisho kati ya mabinti wanne wa Mzee Sepetu.
Wema hakufikiria kama atakuja kuwa mmoja kati ya ma-star wakubwa hapa
nchini hadi nchi za nje mpaka siku mmoja alipo kuwa kwenye matembezi
yake Slypway Masaki alikutana na dada Mange Kimambi na kushawishiwa
ashiriki mashindano ya Miss Tanzania 2006...
Wema Sepetu aliibuka kidedea na kuwagalagaza Jokate Kidoti Mwegelo na Lisa Jensen
Ombi kwa dada Wema ni kwamba achana na Diamond hakufai anataka
kukumaliza tu ili akae pembeni akucheke anatambua kabisa ulimwengu mzima
wote unajua ameng'ara kwa kupitia nyota ya Wema sasa anataka akuzime
ili apate kutawala yeye achana naye bwana fanya ya maendeleo atakutafuta
mwenyewe kwanza mnapo weka story kila siku Wema na Diamond ndio
unamsaidia auze kazi zake maana akitoa nyimbo kila mmoja anataka ajue
safari hii anamwimbia nini Wema yaani hauzi bila ya jina lako kama
umemshtukia akiwa anatoa album au wimbo ndio zinakuja skendo za Wema na
Diamond inamaana ndio muda huo huo anapo tafutia skendo auze yeye kwa
kukupitia mgongo wako.
Kabla ya kuwa miss Tanzania alikuwa na mwandani wake japo hakuwa super
star lakini hawakudumu maana aliposhikilia taji alikuwa busy jambo
lililomfanya akose muda wa kumpa mwandani wake lakini muda mchache
akakutana na Marehemu Kanumba na kuanza uhusiano mara moja....
Uhusiano baina ya Kanumba na Wema ulikwenda vizuri sana nakama mchezo
nyota zao zote zikang'aa sana Kanumba sasa akaonekana Kanumba kweli si
yule wa kwenye maigizo ya kikundi cha Kaole tena uhuu ni ukweli kabisa..
na haswa waliposhirikiana katika movies zao walizidisha umaarufu mara
dufu, lakini kiukweli ni kwamba Kanumba ndiye aliye gundua kipaji cha
Wema na ndiyo aliye muibua katika sanaa ya kuigiza.
Wema sijui ni utundu au utoto au ulimbukeni wa mapenzi basi akamsaliti Marehemu Kanumba na kuwa na mvuta bangi Jumbe.
Pichani ni Wema na mpenzi wake Steven Kanumba enzi za uhai wake Kanumba (RIP)
Kwakweli katika mapenzi yote nazani alipochemsha binti wa Sepetu ni pale
alipokuwa na Jumbe maana ilimpelekea hadi kuwekwa rumande. Natusinge
angalia Wema naye angekuwa mvutaji bangi na madawa ya kulevya
Wema mahakamani akiwa na mpenziwake wa zamani Jumbe
Wazazi wake haswa mama mtu alijitahidi sana kumuokoa Wema kwenye mikono mibaya ya Jumbe
Heka heka za Wema wa Sepetu hazikuishia hapo akajikuta mikononi mwa Chalz Baba kaka yangu na mie huyooo
Wazazi wakaona basi tena maana mwanao kutwa magazetini wakampeleka
Ulayaaaa...sasa akiwa marekani kwa mmoja wa dadazake huko alikuwa
anachati na watu kwa kutumia mitandao ya kijamii hii chating ya kwanza
ya Wema na Diamond ilikuwa kwenye FACEBOOK siku hiyo mtoto wema alikuwa
anacomment kwenye wall ya Diamond kimahaba huku mtoto wa mbagala akijibu
mashambulizi asije poteza bahati
Mara Wema anasema mtu kifudenge naona kachoka a reply sasa hivi
....ikitajwa hivyo Diamond ana jibu akijijua yeye ndio mtukifudenge
Dah! enzi hizo diamond alikuwa kituko jamani hajulikani kabisaaaa watu
mkisikia wimbo mkali wa mbagala mnatafuta aliyeimba nani mnakuta kituko
mnabakia lakini anaimba vizuri.
Wema Sepetu alipotua tu inchini alifikia kupanga na kumkaribisha mpenzi
wake mpya Diamond na kuanza maisha ya pamoja ya raha na mstarehe.....
Kwakweli watanzania wengi walipigwa na butwaa kila mmoja alilalama why
Wema akachukua kinyarika kama hicho na mengi mabaya juu yao.
Nausifu sana ujasiri wa Wema kwani aliweka pamba masikioni na kutaka
kutudhihirishia kuwa Naseeb aliyempenda yeye ni Almasi ...Diamond ambayo
inang'aa duniani kote.
Hapa tunaona kabisa japo Diamond Platnum alishatoka na nyimbo zake kama
mbili hivi kali moja wako ya Mbagala lakini hakuwa juu kiasi hicho na
bila Wema angebakia kama wasanii wengine wanatesa na nyimbo kali ila
nyota hazing'ai kivileee Ben Pol, Chid Benzi Barnaba na wengineo.
Wema hakuona haya kumpenda hadharani Diamond alimpiga mabusu hadharani
watu wakapaka sana domo na mengineyo mengi lakini alizidisha mapenzi
mara dufu. Ndipo tukaanza kumuona Diamond muonekano wa pili aling'aa
sana akawa na swaga za Wema, kiingereza kidogo kila mwanamke akatamani
awe kama Wema na Diamond wakawa hadithi tamu midomoni mwa watu navile
mtoto Wema anavyojua kudeka na kupenda watu wakachanganyikiwa na mapenzi
yao yalivyo noga.
Tutashangaa sana kwanini awali watu hawakupenda na wengine walimcheka
sana Wema kuwa na Diamond lakini sasa jamii nzima inataka kusikia kwamba
Wema amerudiana na Diamond...umeona eheee?
Mtu wa karibu na madam alininyetisha kwamba Wema alimpenda kwa dhati
Diamond japo alipigwa vita sana na jamii kuwa hafai na si wa hadhi yake
lakini hakuvunjika moyo alimpenda zaidi Diamond nakutufanya watanzania
wote na ulimwengu wote kumtambua Diamond na kipaji chake na hadi
tukamuona handsome wakati alikuwa hatazamaniki eti leo hii amekuwa super
star anajidai kumbwaga na kumsaliti tena na kutembea na mashoga wa Wema
kwakweli hii haijakaa sawa kabisa..hatuwezi kuwaacha walale na huyo
kinyago wake Penny asiye kuwa hata na aibu namshangaa bado analazwa
kwenye mashuka ya Wema na anakubali kwanini kama anampenda asimletee
mengine wakalala ndio tuwaache..Diamond ni wa Wema tu labda arudie ule
uchokoraa wake wa zamani wa mbagala ndio tutamucha sasa nao wamchukue
wamng'aishe tuone kama watamgombea tena alisema kwa huzuni mnyetishaji.
Wema Sepetu amezidi kupata umaarufu japo magazeti mengi yakiendelea
kumchafua usiku na mchana lakini ni binti ambaye aseme leo atakuwa
jangwani anayetaka kumuona aje basi hakika maelfu ya watu watakusanyika
hapo nyota yake kwakweli iko juu mno ndio mana kila atakaye mshika mkono
naye lazima awe juu na hii si kwa wanaume wake ni hata mashoga zake wa
kike mfano halisi ni Snura.
Pamoja na Wema kusemwa sana magazetini na kusalitiwa mara nyingi na
kusemwa vibaya na mashoga zake na yote hayo lakini bado yuko juu kwani
binti huyu ana kampuni yake ya production inayoitwa Endless fame na bado
anakipindi chake ambacho hivi karibuni kinategemewa kurushwa hewani
kitakachoitwa Reality Show na anajiweza imaisha na Mungu anazidi
kumbariki kwani anajitoa sana kwa watu na sadaka, anamiliki nyumba na
magari kwakweli Wema Sepetu you shine like diamond... your a star isiyo
fifia.
CHANZO;MASAMA BLOGS
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni