TANGAZO

TANGAZO

Jumamosi, 12 Desemba 2015

ROONEY ATAKIWA CHINA KWA GHARAMA KUBWA HAIJAWAHI KUTOKEA...........




   
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amepewa ya Pauni Milioni 75 kwenda kuungana na kocha Sven Goran Eriksson nchini China.
 
Ligi Kuu ya China inamtaka mshambuliaji huyo wa Manchester United akawe nyota wao mpya, na ipo tayari kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 25 kwa msimu.
 
Hivyo kituo kipya cha kazi cha Rooney akiamua kuondoka Old Trafford — kinaweza kuwa Shanghai SIPG, ambayo iko chini ya kocha wa zamani wa England, Eriksson.


 Kititia cha malipo kitahusisha haki ya matumizi ya picha ambayo itamuwezesha Rooney kupata fedha nyingi zaidi iwapo ataisaidia kukua kwa umaarufu wa CSL (Ligi Kuu ya China).
 
CSL, ambayo pia inamtaka Nahodha wa Chelsea, John Terry, inataka Rooney ambaye amebakiza Mkataba wa miaka mitatu Man United, ajiunge nao haraka iwezekanavyo 
Chanzo:ASANTE MUYA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni