Waasi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan tawi la kaskazini (SPLM-N)
wamedai kuwa wameua askari 13 wa jeshi la nchi hiyo, katika jimbo la
Blue Nile.
Msemaji wa harakati hiyo Arno Nugutlu Lodi amesema kuwa hadi sasa
wameshaua wanajeshi 13 wa serikali ya Sudan na kuzima hujuma zao katika
eneo la Torda, kaunti ya Bau katika jimbo la Blue Nile.
Amesema walifanikiwa kuzima uvamizi wa jeshi la Sudan katika mapigano yaliyojiri kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 7 adhuhuri Jumamosi iliyopita.
Msemaji wa SPLM-N amedai kuwa askari wa serikali waliosalia walilazimika kukimbilia usalama wao kupitia Mto Maganza, yapata kilomita 45 kusini mwa mji wa Damazin.
Hata hivyo Msemaji wa jeshi la Sudan amekataa kulizungumzia suala hilo alipotakiwa kufanya hivyo na vyombo vya habari.
Mwishoni mwa mwezi uliopita wa Novemba, mazungumzo ya kusaka amani kati ya pande mbili hizo yalimalizika bila ya kufikiwa natija yoyote. Umoja wa Afrika AU umekuwa ukijaribu kuzipatanisha pande hizo hasimu bila ya mafanikio yoyote.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni