TANGAZO

TANGAZO

Jumatano, 30 Desemba 2015

SAMATTA: NGUVU YA MASHABIKI ILINIFANYA NISAJILIWE TP MAZEMBE

Rais wa TP Mazembe Moise Katumbi (katikati) akiwa kazungukwa na kundi kubwa la mashabiki wa timu hiyo

Rais wa TP Mazembe Moise Katumbi (katikati) akiwa kazungukwa na kundi kubwa la mashabiki wa timu hiyo
Tunaendelea na ‘Safari Ndefu ya Mbwana Samatta kutoka Mbagala kwenda Ulaya’ jana tuliangalia namna ambavyo Samatta alitoka African Lyon akajiunga na wekundu wa Msimbazi Simba pamoja na maisha yake yote akiwa Simba. Leo tunaangalia namna alivyojiunga na timu ya TP Mazembe ambayo ndiyo imemtambulisha kwenye soka la Afrika na duniani.
Samatta anasema nguvu ya mashabiki ndiyo iltumika kumsajili yeye na haikuwa pendekezo la mwalimu wala rais wa timu hiyo

“Mashabiki ambao walikuja Bongo kwenye mechi ya Simba na TP Mazembe ndio ambao walipeleka ripoti kwa bosi kwamba mchezaji flani mzuri na tunataka aje acheze kwenye timu yetu. Walikuwa na nguvu kubwa kwsababu bosi wa timu Moise Katumbi ni mtu ambaye anasikiliza sana mashabiki”, alisema Samatta wakati akifanya mahojiano maalum na mtandao huu.
“Kwahiyo baada ya mamshabiki kumfikishia Katumbi hilo suala hakubisha akasema ninunuliwe kwasababu anapesa”.
Moja ya mashabiki ambao wamechangia Samatta kusajiliwa na TP Mazembe ni Mario Kamweli ambaye anasema yeye ndiyo alimuona Samatta kwa mara ya kwanza akaenda kwaambia mashabiki wenzake habari za Samatta na walipo kuja Bongo kucheza dhidi ya Simba wakakubali uwezo wa Samatta na kutaka asajiliwe na timu yao.
“Mimi ndiyo nilimuona nikaenda kuwaambia wenzangu na tulipokuja kucheza mechi wakamuona wakasema kweli anafaa kucheza kwenye timu yetu”, amesema Kimweli.
Timu ya shaffihdauda.co.tz imepiga story pia na rais wa timu ya TP Mazembe Moise Katumbi juu ya maisha ya ma-star wa bongo wanaokipiga kwenye timu yake na hakusita kufunguka juu ya nidhamu ya juu inayooneshwa na nyota hao wa Tanzania.
Katumbi alifika mbali zaidi pale aliposema kwamba, kama wachezaji wote wa kiafrika wangekuwa na nidhamu kama ya Samatta na Ulimwengu basi soka la Afrika litafika mbali sana.
“Kiwango cha Samatta pamoja na Ulimwengu kinatokana na nidhamu. Wananidhamu ya juu sana kwenye timu, huwezi kusikia tatizo kutoka kwa Samatta wala Ulimwengu. Hawa ni kama watoto wangu, kama wachezaji wote wa kiafrika wangekuwa na nidhamu kama waliyonayo wachezaji hawa, basi soka la Afrika lingefika mbali sana”, hayo ni maneno ya Moise Katumbi Rais wa TP Mazembe.
Angalia video hapa chini jinsi mashabiki wa Mazembe wanavyoelezea walivyopambana kuhakikisha Samatta anatua kwenye timu yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni