Ikiwa ni siku kadhaa tangu Rais wa awamo ya tano Dk.John Magufuli kutoa tamko la hakutakua na sherehe za kitaifa December 9 na badala yake watu watatumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao.
Sasa time hii headlines za usafi
zimewagusa wasanii na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda
ambapo tarehe 9 December wataungana kuhakikisha
wilaya ya Kinondoni
usafi unafanyika kwenye maeneo mbalimbali.
Akiongea na mwandishi wa habari Steve Nyerere alisema..’Kutakuwa
na wasanii mbalimbali ambao tutaungana siku ya usafi katika wilaya ya
Kinondoni pamoja na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, watu wengi wanaamini
usafi ni lazima ma hospitali lakini usafi unaanzia nyumbani kwako,
masoko na sehemu mbalimbali zinazomzunguka mwanadamu’ – Steve Nyerere
‘Napenda
kusema kwamba siku hiyo wasanii pamoja na wananchi tujitokeze kutekeleza
kile kilichosemwa na Mh Rais wa awamo ya tano Dk.John Pombe Magufuli
tujitokeze kwa wingi kufanya usafi huu ni mfano wa kuigwa kwenye
mataifa haya ya Afrika’>> Steve Nyerere
‘Wapo
wasanii kama 180 mimi nikiwa kama kiongozi wao na Mh DC Paul Makonda
tumechagua wasanii mbalimbali wakiwemo wasanii wa Bongo Movie, Bongo
Fleva, wanenguaji kwa hiyo tumechagua vitengo vyote vya sanaa
kuhakikisha usafi unafanyika katika wilaya ya Kinondoni’>> Steve Nyerere
Chanzo: Millardy Ayyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni