Jamaa anaitwa DJ Young Guru, huyu ndio jamaa ambae anafanya kazi kama DJ wa rapper Jay Z akiwa kwenye show zake… Hii ni safari ya pili kwa Young Guru kukanyaga Tanzania.
Young Guru
anasema anajisikia poa sana kwa sababu tayari alipata washkaji kadhaa
alipotua mara ya kwanza na alifahamiana pia na baadhi ya watu, kwa hiyo
sio mgeni kabisa safari hii.
Kingine ni kwamba kinachompa furaha zaidi ni kuwa ndani ya Tanzania akiburudisha watu wa nguvu katika usiku wa Grown & Sexy December 31 2015 wakati wa mkesha na party ya kuupokea mwaka mpya 2016 !!
Jamaa anakumbuka pia baadhi ya washkaji zake yuko pia rapper Mwana FA, enjoy na interview yote dakika zake tatu baada ya kutua Uwanja wa ndege Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni