Aliyekuwa waziri mkuu wa Burkina Faso Roch Mark Christian Kabore, anaapishwa leo kama rais nchi hiyo .
Bwana
Kabore ambaye alishinda uchaguzi wa mwezi uliopita, alikuwa mshirika wa
karibu wa rais wa zamani Blaise Compaore, ambaye alinyakua mamlaka
baada ya mapinduzi ya jeshi, na kutawala taifa hilo kwa miaka 27 hadi
mapinduzi ya umma mwaka uliopita.Kabore alitofautiana na Compaore mwaka uliopita alipotangaza nia ya kuendelea kuongoza.
Viongozi wa mataifa 5 ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwake.
Tangu ijinyakulie uhuru kutoka kwa Ufransa mwaka wa 1960 Viongozi wengi wa Burkina Faso wamekuwa wakijinyakulia uongozi kwa mtutu wa bunduki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni