December 30 ilikuwa ni siku ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta kukutana na uongozi wa wizara ya habari, vijana, utamaduni, burudani na michezo Nape Nnauye
.
Mshambuliaji huyo ambaye anahusishwa kwenda kucheza soka la kulipwa katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji aliomba kukutana na waziri Nape
ili kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa waziri wa wizara inayomuhusu na
kuomba baraka kuelekea fainali ya tuzo za mchezaji bora wa Afrika
zitazofanyika January 7 Abuja Nigeria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni