TANGAZO

TANGAZO

Jumanne, 29 Desemba 2015

Waasi wa Rwanda wapigana na Maimai nchini DRC


Waasi wa Rwanda wapigana na Maimai nchini DRC
Kumezuka mapigano baina ya waasi wa Rwanda na Maimai mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Watu kadhaa wameripotiwa kuuawa kwenye mapigano hayo.
Shirika la habari la Xinhua limeripoti habari hiyo na kuzinukuu duru za ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikisema kuwa, watu saba wameuawa katika mapigano baina ya waasi wa Rwanda wa FDLR na wale wa Maimai wa UPDI mkoani Kivu Kaskazini.

Duru hizo zimeongeza kuwa, waasi wa Rwanda ndio walioanza kuishambulia kambi ya wakimbizi wa Maimai kusini mwa eneo la Lubero huko Kivu Kaskazini.
Maafisa wa jeshi la Kongo wamesema kuwa wanajeshi wa nchi hiyo wametumwa kwenye eneo la Lubero kwa ajili ya kutuliza hali ya mambo na kuimarisha amani.
Mkoa wa Kivu Kaskazini una utajiri mkubwa wa madini na hiyo inatajwa kuwa sababu ya kuzuka mapigano ya mara kwa mara kati ya makundi mbalimbali mkoani humo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni