TANGAZO
Jumanne, 29 Desemba 2015
PETR CECH AMEWEKA REKODI MPYA YA KUKUMBUKWA EPL
Petr Cech amevunja rasmi rekodi ya kuwa kipa aliyecheza mechi nyingi bila ya kufungwa ‘clean sheets’ katika historia ya Ligi Kuu Engalnd.
Cech, 33, amevunja rekodi ya David James baada ya kufikisha idadi ya ‘clean sheets’ 170 katika mchezo wa jana usiku dhidi ya Bournemouth ambapo Arsenal walishinda kwa magoli 2-0.
Amefikisha idadi hiyo ndani ya michezo 352 dhidi ya 572 ya Davidi James ambaye alikipiga kunako klabu za Liverpool, Aston Villa, West Ham, Manchester City na Portsmouth.
“Anaweza kujivunia sana kwa hili kutokana na kuwa ni mafanikio ya kukumbukwa sana”, Wenger alisema. “Ni kipa aliyejaaliwa sana yule”.
Arsenal wamekwea kileleni mwa ligi baada ya ushindi wa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa na Gabriel na Mesut Ozil, lakini hata hivyo wanaweza kupitwa na Leicester City endapo wataifunga Manchester City leo usiku.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni