Pamoja na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya
England Chelsea kupoteza matumaini ya kutwaa ubingwa kwa mara nyingine
lakini kocha wao mpya Guus Hiddink ana mipango mingine ya ushindi.
Baada ya ushindi wa jana wa mabao 3-0 Hiddink
amesema klabu yake hiyo inaweza kumaliza ligi hiyo ikiwa katika nafasi
nne bora za juu mwishoni mwa msimu huu.
Klabu hiyo ya Stamford Bridge imeenda mechi nne bila kufungwa, kwa mara ya kwanza msimu huu, na kupanda hadi nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.
Hata hivyo, bado wanapungukiwa na alama 13 kuweza kufuzu kcheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Alisema ligi ni ngumu lakini pia ni rahisi kushinda hivyo watapambana kuhakikisha wanashika nafasi za juu.
Hiddink alichukua nafasi ya kuifundisha timu
hiyo kwa muda baada ya kocha wa awali Jose Mourihno kuondolewa kutokana
na mwenendo mbaya wa timu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni