Mabingwa wa Tanzania Bara Timu ya
Yanga, imefanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali kufuatia ushindi wa Bao
2-1 dhidi ya Mtibwa mabao ambayo yamefungwa na wachezaji Aboubakar na
Malimi Busungu na kuwa kinara wa kundi B la michuano ya kombe la
Mapinduzi baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 7.
Katika mchezo mwingine wa mapema kutinga hatua ya nu Nusu Fainali Timu ya Mafunzo imeichapa Azam FC 2-1 kwa ushindi usio na faida kwa timu hiyo baada ya kutupwa nje ya mashindano hayo kwa uchache wa pointi.
Yanga sasa watacheza Nusu Fainali na Mshindi wa Pili wa Kundi A na Mtibwa Sugar kukutana na Mshindi wa Kundi hilo.
Kundi A linamaliza Mechi zake leo Ijumaa kwa Timu ya Jamhuri kuchuana na URA na Simba ikicheza na JKU huku kila Timu ikiwa ina nafasi kutinga Nusu Fainali ikipata matokeo mazuri ingawa Sare kwa Simba itawafikisha Nusu Fainali wakati URA na Jamhuri zikihitaji ushindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni