OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA – TAMISEMI
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA – TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface
Simbachawene (Mb) kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 2(2) cha
Amri ya kuanzisha Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), (The
Executive Agencies) (The Dar Rapid Transit Agency) (Establishment) Order
) Tangazo la Serikali namba 120 la 2007, amemteua Mhandisi Ronald
Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Mabasi Yaendayo Haraka
Dar es salaam (DART) kuanzia tarehe 04/01/2016.Uteuzi huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Bibi Asteria L. Mlambo tarehe 23/12/2015. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Ronald Lwakatare alikuwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) akishughulikia Ufuatiliaji na Tathmini. Mhandisi Lwakatare anatakiwa kuripoti na kuanza kazi mara moja.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Januari 05, 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni