Tetesi za kupewa kwa Jose Mourinho na klabu ya Manchester United zinazidi kushika hatamu kila dakika.
Gazeti la kila siku El Confidencial leo limeripoti taarifa za ndani za
mkataba unaosubiriwa kusainiwa baina ya Jose Mourinho na waajiri wake
wapya Manchester United.
Taarifa za ‘Special One’ kubeba mikoba ya Van Gaal zimechapishwa na kila chombo cha habari huko England asubuhi ya leo.
Vichwa vya habari vya magazeti vimeandika kwamba: Jose Mourinho
amewaambia marafiki wa karibu kwamba atakuwa boss mpya wa United kuanzia
msimu ujao.
Kwa
mujibu wa El Confidencial, wakati dili la kumleta Mourinho likiwa
linamaliziwa katika hatua za mwisho, wakala wa kocha huyo Jorge Mendes
na timu yake ya wanasheria kwa sasa wanaripotiwa kuwa kwenye kumalizia
majadiliano ya vipengele vya mwisho na Red Devils.
Taarifa zaidi kutoka kwenye sehemu ya mkataba wa Mourinho na United
ni kwamba mkataba utakuwa wa kuanzia msimu wa 2016/17 mpaka 2019/20,
huku akiweka kibindoni kiasi cha 20 million euros kwa mwaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni