TANGAZO

TANGAZO

Ijumaa, 5 Februari 2016

Taarifa kamili iliyonifikia kutokea bungeni kuhusu Watanzania kuvamiwa na kuuawa India…(+Audio)



Stori ya Wanafunzi wa Tanzania kuvamiwa na kupigwa huku mmoja wa wasichana akivuliwa nguo na kutembezwa barabarani imechukua headline nyingi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari haswa hapa nchini, uzito wa tukio hili umefika bungeni Dodoma, Na hapa Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk. Augustine Mahiga ana haya ya kusema.
Jana nilitoa taarifa ya awali kuhusu wanafunzi wa Kitanzania walipingwa na msichana mmoja alivuliwa  nguo na kutembezwa barabarani nchini India, taarifa tulizozipata ni kweli kitendo kilitokea

lilitokea tukio la mwanafunzi wa Kisudani kuzigonga pikipiki tatu na pia kumgonga mama wa Kihindi ambaye alifariki hapohapo, baada ya tukio mwanafunzi huyo akakimbia
Wananchi wa India waliamua kuchoma gari hilo, lakini baada ya muda gari jingine lilifuata likiwa na wanafunzi  wanne wa Tanzania akiwemo msichana mmoja. Walilisimamisha lile gari na kuwavuta wanafunzi wale kisha kuwapiga na kuchoma gari lao
Hatua gani zimechukuliwa hadi sasa?Tumemweleza Balozi wa India hapa nchini na akachukua hatua ya kuielezea Serikali yake, na hadi sasa watuhumiwa wote wamekamatwa na wamepelekwa Mahakamani. ” Waziri Mahiga
Pia jana nilieleza kwamba kuna mwanafunzi mmoja alifariki karibu na eneo lilipotokea hilo tukio, taarifa za awali zilikuwa zinatatanisha tukazani kifo chake kinahusishwa na tukio hilo la uvamizi, lakini sio kweli.. Mtanzania huyo alikuwa anaendesha pikipiki akapata ajali na kufariki palepale  
Unaweza pia kumsikiliza kwenye hii sauti hapa chini video ya tukio lililo tokea India

Chanzo:Millardy Ayyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni