TANGAZO
Ijumaa, 5 Februari 2016
BABA WA NEYMAR AFICHUA DAU LILILOTENGWA NA MAN UTD KWA AJILI YA MWANAE
Baba mzazi wa mchezaji wa Barcelona, Neymar Jr wiki hii amefichua siri juu pesa ya ambayo klabu ya Manchester United waliyoitenga msimu uliopita kutaka kumsajili mtoto wake kutoka Barcelona, huku wakiwa tayari kukidhi buyout clause iliyowekwa na Barcelona ya pauni 145m ili kumnasa mbrazili huyo.
Neymar Snr ambaye amemsindikiza mwanae katika kesi inayowakabili ya kutoweka wazi kiasi sahihi cha pesa ambayo FC Barcelona walitoa kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Santos ya Brazil, amesema kuwa Manchester United walitenga mezani mamilioni hayo ya fedha kumtaka mwanae lakini akasisitiza kuwa hajui kitakachotokea mbeleni, ila bado kijana wake ana mkataba wa misimu 2 na ana furaha Nou Camp.
Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal aliweka wazi kutaka kuongeza ubunifu katika eneo la mwisho la kiwanja (ushambuliaji) huku akiwa yuko tayari kutoa pesa hizo pamoja na kuwa tayari Van Gaal amekwisha tumia pauni 205m katika kipindi cha miezi 18.
Endapo United wangefanikiwa kumsajili Neymar Jr kwa ada hiyo, ingemfanya Neymar Jr kuwa ndiye mchezaji ghali zaidi kwa uhamisho duniani na kuipiku rekodi inayoshikiliwa na Gareth Bale ya pauni 85.1m akitokea Tottenham Hotspur kwenda Real Madrid.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni