February 18 baraza la mitihani Tanzania
NECTA wametangaza matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2015 yafuatayo ni
maneno matatu waliyosemwa na katibu mtendaji wa baraza la mitihani
Tanzania NECTA Dk Charles Msonde.
“Katika
mkutano maalum wa baraza wa 110 uliofanyika February 17 2016, baraza la
mitihani Tanzania lilipitia taarifa ya matokeo ya kidato cha nne na
maarifa uliofanyika tarehe 2 hadi 27 November 2015 na kuidhinisha
kutangaza rasmi kwa matokeo hayo katika mitihani ya kidato cha nne 2015”
“Jumla
ya watahiniwa 448382 waliandikishwa kufanya mtihani huo, wasichana ni
229144 na wavulana 219238 kati ya hao watahiniwa waliosajiliwa,
watahiniwa wa shule walikuwa 394o65, wakati watahiniwa wa kujitegemea
walikuwa 54317”
“Watahiniwa
wa shule asilimia 96.71 walifanya mitihani na watahiniwa 14749 ambao
sawa na asilimia 3.29 hawakufanya mtihani, watahiniwa wa kujitegemea
49333 sawa na asilimia 90.82 lakini watahiniwa 4984 sawa na asilimia
9.18 hawakufanya mtihani”
“Watahiniwa
wa mtihani wa maarifa 19547 waliosajiliwa, lakini watahiniwa kati ya
wale waliosajili 16162 sawa na asilimia 82.68 walifanya mtihani, lakini
watahiniwa 3385 kati ya hao hawakufanya mtihani”
“Kwa
jumla ya watahiniwa 272947 sawa na asilimia 67.53 ya watahiniwa
waliofanya mtihani wa kidato cha nne wamefaulu mtihani, wasichana
waliofaulu ni 131913 sawa na asilimia 64.84, wakati wavulana waliofaulu
ni 141034 sawa na asilimia 71.09”
“lakini
mwaka jana watahiniwa waliofaulu walikuwa 196805 sawa na asilimia 68.
33 hivyo ufaulu ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana, ufaulu umeshuka
kwa asilimia 0.8 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2014”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni