Kushoto ni Diwani wa kata ya Ubungo anayemaliza muda wake, Boniface Jacob akisindikizwa na Afisa usalama wa jeshi la polisi.
Diwani
wa kata ya Ubungo anayemaliza muda wake, Boniface Jacob leo
amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam
akituhumiwa kumpiga na kumjeruhi mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru,
Christopher Lisso.
Mbele
ya hakimu Hellen Liwa, wakili wa serikali Kenneth Setwao alisema
Septemba 11, 2015 katika Wilaya ya Kinondoni mtuhumiwa alitenda makosa
mawili.
Katika
kosa la kwanza Setwao alisema mtuhumiwa alimpiga mwandishi wa habari wa
gazeti la Uhuru, Christopher Lisso na kumsababishia maumivu sehemu
mbalimbali za mwili wake.
Alisema
katika shitaka la pili mtuhumiwa anatuhumiwa kuharibu kamera yenye
thamani ya Sh8 milioni, mali ya kampuni ya Uhuru Publications Limited.
Mtuhumiwa
anayetetewa na wakili wa kujitegemea, John Mallya amekana mashtaka yote
mawili na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza matakwa yaliyowekwa ya
kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi yenye thamani ya Sh8 milioni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni