KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani,
Papa Francis jana alieleza mabadiliko mapya yanayolenga kuwarahisishia
Wakatoliki kuvunja ndoa zao na kuoa upya.
Dhamira hiyo ni ishara nyingine ya
dhamira ya Papa huyo kutaka kulifanya Kanisa Katoliki liwe rafiki zaidi
na kuendana matakwa ya walio wengi.
Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Papa
alisema si haki kwa wenzi kuishi muda mrefu ‘wakikandamizwa na wingu la
shaka’ kuhusu uhalali wa ndoa zao.
Ikumbukwe kwamba ni msimamo wa Papa
kumkatalia Mfalme Henry the VIII wa Uingereza kumtaliki mkewe Catherine
wa Aragon katika karne ya 16 uliosababisha England ijitenge na Rome na
kushuhudia kuundwa kwa Kanisa la England huku mfalme akiwa mlinzi wa
Imani wa kanisa hilo.
Mabadiliko makuu matatu aliyotangaza
Papa jana ni kuondoa mchakato wa mapitio ya mara ya pili wa uamuzi wa
kutoa talaka kupitia mahakama ya kanisa kabla ya ndoa kuvunjwa.
Mengine ni kuwapatia maaskofu uwezo wa
kuharakisha na kuvunja ndoa wenzi wanapoamua wenyewe katika mazingira
fulani kama vile ukatili katika ndoa au uasherati na mchakato huo wa
talaka kuwa bure, isipokuwa kwa kulipa ada ndogo kwa ajili ya gharama za
utawala.
Kabla ya sheria hiyo, Wakatoliki
waliotaka talaka walihitaji kibali kutoka kwa mahakama mbili za kanisa,
wakati sheria mpya inabakiza moja ingawa rufaa bado zinaruhusiwa.
Kabla ya sheria hiyo, wanandoa wa
Wakatoliki wanaotalikiana bila idhini ya kanisa na kuolewa upya
walihesabiwa kama wazinifu na hawakuruhusiwa kupokea komunio.
Lakini kwa mujibu wa utaratibu mpya, wanaotalikiana wakioa au kuolewa tena watabakia kuwa wafuasi wa kanisa hilo.
Mwaka jana Papa aliunda tume ya
wanasheria wa kanisa hilo kuboresha na kurekebisha taratibu hizo
kurahisisha wanandoa kuachana na kupunguza gharama.
Mageuzi hayo yalikuja katika mfumo wa nyaraka mbili zinazoitwa ‘motu proprio’, neno la kilatini lililobuniwa na Papa mwenyewe.
Taratibu hizo zitakuwa rasmi kama sehemu
ya sheria za kanisa (canon law) ifikapo Desemba 8 mwaka huu wakati Papa
atakapoanza kutangaza Mwaka wa Jubilee ambao kwa kawaida huhusishwa na
msamaha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni