TANGAZO

TANGAZO

Jumapili, 6 Septemba 2015

WAYNE ROONEY AMWAGA SIFA KWA MESSI HIKI NDICHO ALICHO KISEMA

ESSI
 Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza na Manchester United Wayne Rooney amefikia rekodi ya mkongwe wa Uingereza Sir Bobby Charlton ingawa kwa penati. Rooney ameweza kufikia rekodi hiyo ya magoli kwa akiwa kwenye mechi na San Marino baada ya England kushinda kwa 0-3.

Mechi hiyo ambayo Rooney alishuhudiwa na mkewe na wanae pia imetengeneza headline nyingine baada ya Rooney kumzungumzia vizuri Messi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 analinganisha hali yake ya kukosa kombe la dunia kama Lionel Messi wa Argentina.
Rooney alisema “Tangu miaka iliyopita watu walikua wanasema Messi sio Maradona sababu Messi hajachukua kombe la dunia, ila kwa upande wangu Messi ni mchezaji mzuri kuliko Maradona. Ila hivyo ndivyo mpira ulivyo”.
Aliongezea “Mkiwa kama timu, mnajadiliwa kutokana na makombe mliyochukua, Sir Bobby amefanya hivyo. Nina matumaini bado kuna muda na mimi kuweza kufikia mafanikio kama yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni