TANGAZO
Jumanne, 22 Machi 2016
Man City kuanza zama za Guardiola kwa kusajili wachezaji wanne au watano wenye majina makubwa
Viongozi wa City wanaamini mazingira mazuri ya kazi,
na nguvu ya usajili vitamshawishi meneja wao mpya kudumu klabuni zaidi
ya miaka mitatu
Manchester City watampa
Pep Guardiola ushirikiano kwa asilimia mia moja katika mkakati wa
kuunda kikosi imara kwa kusajili wachezaji wanne au watano wenye majina
makubwa majira ya joto,Inaaminika kuwa simu za mkononi za Guardiola na Mkurugenzi wa michezo wa City Txiki Begiristain zimekuwa zikipokea simu nyingi kutoka kwa mawakala wa wachezaji wenye uwezo mkubwa kutoka Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Bundesliga na kwingineko.
Conte akanusha vikali tetesi za kibarua cha Chelsea
Kocha huyo wa Italia amehusishwa vikali na tetesi za
kutua Darajani Stamford lakini yeye amesisitiza kuwa akili yake yote ipo
pamoja na Azzurri kuelekea Euro 2016
Kocha huyo wa Italia Bw. Antonio Conte amekanusha taarifa hizo zinazodai kuwa anakaribia kuwa meneja wa Chelsea, akisisitiza kuwa akili yake ipo kwenye kibarua chake cha timu ya taifa inayojiandaa na michuano ya Euro 2016.
Jumatatu, 21 Machi 2016
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)