TANGAZO

TANGAZO

Jumanne, 22 Machi 2016

Conte akanusha vikali tetesi za kibarua cha Chelsea


Conte akanusha vikali tetesi za kibarua cha Chelsea
Kocha huyo wa Italia amehusishwa vikali na tetesi za kutua Darajani Stamford lakini yeye amesisitiza kuwa akili yake yote ipo pamoja na Azzurri kuelekea Euro 2016
Kocha huyo wa Italia Bw. Antonio Conte amekanusha taarifa hizo zinazodai kuwa anakaribia kuwa meneja wa Chelsea, akisisitiza kuwa akili yake ipo kwenye kibarua chake cha timu ya taifa inayojiandaa na michuano ya Euro 2016.

Conte amekuwa mstari wa mbele kati ya wanaotajwa kumrithi Guus Hiddink Darajani majira ya joto na alitangaza juma lililopita kuwa hataendelea tena kama bosi wa Italia baada ya michuano itakayofanyika Ufaransa.

Akizungumzia mechi za kimataifa za kirafiki dhidi ya Hispania na Ujerumani zilizo mbele yake, Conte amesisitiza kuwa tetesi za kibarua hicho cha timu ya Ligi Kuu ya Uingereza haziwezi kumvuruga katika kazi yake anayoifanya sasa.

"[Kwenda] Uingereza? Hakuna kinachonichanganya kwa sasa. Akili yangu ipo kwenye timu ya taifa," alisema.

"Uzoefu huu umenisaidia kujiimarisha.

"Umekuwa ni uzoefu mzuri usio wa kifani, Daima nimekuwa nikiwahusudu makocha walioiwakilisha Italia.Sasa ni zamu yangu, na ninafurahi sana. Tutaendelea na kazi nzuri kama kawaida."

Conte pia alitetea uamuzi wake wa kuacha kibarua hicho baada ya michuano, ingawa anakiri kwamba alipata wakati mgumu kufanya uamuzi huo

"Nilikuwa sawa na sahihi kabisa kwa sababu zote, baada ya kuulizwa kuelezea nafasi yangu baada ya Euro, kwani mkataba utakuwa umekwisha moja kwa moja," alieleza.

"Nilitafakari vizuri juu ya uamuzi wangu na nilipojiridhisha kwa asilimia 100 kuhusu hisia zangu nilimtaarifu [Rais wa FIGC, Carlo] Tavecchio - mtu aliyenipa kazi hii. Nilimtaarifu kuhusu uamuzi wangu kwa unyenyekevu.

"Nilipata wakati mgumu kwani ni vigumu kuachana na kundi ambalo nafanya nalo kazi nzuri sana.

"Nataka kuusikiliza moyo wangu, kama nilivyofanya nilipoikubali kazi ya Italia."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni