TANGAZO

TANGAZO

Jumanne, 22 Machi 2016

Man City kuanza zama za Guardiola kwa kusajili wachezaji wanne au watano wenye majina makubwa

Man City kuanza zama za Guardiola kwa kusajili wachezaji wanne au watano wenye majina makubwaViongozi wa City wanaamini mazingira mazuri ya kazi, na nguvu ya usajili vitamshawishi meneja wao mpya kudumu klabuni zaidi ya miaka mitatu
Manchester City watampa Pep Guardiola ushirikiano kwa asilimia mia moja katika mkakati wa kuunda kikosi imara kwa kusajili wachezaji wanne au watano wenye majina makubwa majira ya joto,

Inaaminika kuwa simu za mkononi za Guardiola na Mkurugenzi wa michezo wa City Txiki Begiristain zimekuwa zikipokea simu nyingi kutoka kwa mawakala wa wachezaji wenye uwezo mkubwa kutoka Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Bundesliga na kwingineko.

Wakuu wa Etihad pia wanatamani kufanya kila kinachowezekana kumshawishi meneja huyo kudumu klabuni hapo zaidi ya miaka mitatu mara atakapoanza kutumikia mkataba wake utakaoanza Juni 1 iwe timu itafuzu ligi ya Mabingwa ama la!

Mahali ilipo klabu hiyo katika msimamo wa Ligi Kuu ni sehemu ambayo haikutarajiwa na ni kinyume kabisa na malengo kulingana na nguvu ya klabu.

Vijana hao wa Manuel Pellegrini walibaki wakiwa wamekata tamaa wakijitazama mabegani baada ya kuadhirishwa na Mashetani Wekundu kwa kipigo cha 1-0 katika uwanja wa nyumbani, ni dhahiri tumaini lao la ubingwa Ligi Kuu Uingereza limepepea na kuondoka zake.

Lakini mipango madhubuti kwa ajili ya msimu ujao imeshaanza kusukwa na idadi kadhaa ya wachezaji bora wenye majina ikiwa imeshaanza kuorodheshwa kwa ajili ya kuunda kikosi kitakachotumiwa na Pep Guardiola.

Vyanzo vya Goal vimebaini kuwa mchakato wa kumsajili Ilkay Gundogan, kiungo wa Borussia Dortmund unakaribia kukamilika. Wakala wake alikutana na Begiristain katika hoteli ya Amsterdam mapema mwezi Machi na Juventus na Barcelona zimejitoa kwenye mbio za kumfukuzia.

Lakini pia City wapo katika harakati za kumsajili nyota wa Juventus Paul Pogba, ambaye aliondoka United 2012 baada ya kushindwa kupata namba kikosi cha kwanza chini ya Sir Alex Ferguson, wakati kiungo wa Real Madrid Toni Kroos ambaye alifanya kazi chini ya Guardiola msimu mmoja akiwa Bayern Munich anaweza kuivutia City katika usajili wa majira ya joto.









 Blues wametumia paundi milioni 75 kusajili mabeki wa kati misimu miwili iliyopita, ikiwa ni pamoja na Eliaquim Mangala na Nicolas Otamendi kutoka Porto na Valencia, lakini wanajipanga kuingia sokoni na fedha za kutosha kuwasajili John Stones wa Everton na Aymeric Laporte wa Athletic.

Wachezaji makinda wa klabu hiyo pia wanaandaliwa kuchukua nafasi za wachezaji wanaoonekana kuwa wakongwe, ikiwa ni viungo wa Hispania Manu na Aleix Garcia pamoja na Tosin Adarabioyo aliyekulia Manchester kuunda kikosi cha kwanza msimu ujao.

Jason Denayer anatarajiwa kurejeshwa kutoka Galatasaray anakotumika kwa mkopo, ambako amekuwa akicheza kama beki wa kulia, Brahim Diaz kinda mahiri wa miaka 16 atacheza msimu ujao kwenye mechi za Kombe la Ligi.

City wana imani kubwa Guardiola atafanya kazi nzuri ambazo Roberto Mancini na Pellegrini hawakuweza kufanya na kuipa City sifa kubwa katika jiji la Manchester.

Guardiola aliweka misingi thabiti ya Barcelona inayotamba katika soka la Ulaya, hata kama ameshindwa kufanya hivyo Bayern Munich iwe atatwaa taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu au la, lakini pia ameimarisha mbinu za mashambulizi katika Allianz Arena kwa kipindi alichodumu klabuni hapo.

City watafaidi kama meneja huyo atafanikiwa kufikia vilele hivyo kwa wakati atakaodumu Uingereza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni