TANGAZO
Jumatano, 29 Julai 2015
DK SLAA, TUNDU LISSU NA MNYIKA KUIHAMA CHADEMA? HAWAKUWEPO KUMPOKEA LOWASSA
TETESI ZILIZO ENEA KWA WINGI NA HUENDA ZIKAWA KWELI NI KUHUSIANAN NA LISSU
Jumatatu, 6 Julai 2015
Ally Kiba alivyopanda daladala kukutana na mashabiki Dar es salaam, akaulizwa kuhusu Diamond
Tazama video ya alikiba akijibu maswali ya abilia kwenye daladala kutazama bofya
Video ikionyesha walichokifanya Abdu Kiba na Ruby nyuma ya Camera!
Ni dakika chache ambazo zinakutangulizia kuona kitachofata kwenye
video mpya ya Abdu Kiba ft. Ruby (Ayaya) ambayo ni single mpya kwenye
radio kwa wiki kadhaa sasa hivi.
Location ya hii video ni White Sand Dar es salaam Tanzania.
KUTAZAMA VIDEO HII BOFYA
Location ya hii video ni White Sand Dar es salaam Tanzania.
KUTAZAMA VIDEO HII BOFYA
KESHI ATUPIWA VIRAGO NIGERIA
Shirikisho la Soka nchini
Nigeria limetangaza kumsitishia ajira ya kuinoa timu ya Taifa ya Nigeria
‘The Super Eagles’ kocha Steven Keshi.
Siku saba za urais ndani ya CCM
Dar/Dodoma. Ni wiki ngumu kwa Chama cha
Mapinduzi (CCM). Ndivyo unavyoweza kusema kwani chama hicho
kinachotawala kitafanya vikao vyake vya juu vitakavyohitimishwa kwa
kumpata mgombea wake wa urais.
Kikwete: Msimchague huyu
Tanga. Rais Jakaya Kikwete amewataka viongozi
wa dini nchini kuwahimiza waumini wao kuwachagua wanasiasa wasiokuwa
waovu, wasiofanana na uovu au hata kuukaribia.
Amewataka kuepuka makundi ya kisiasa na wasiwape
mwanya wanasiasa wenye dhamira ovu katika kutafuta madaraka kwa thamani
yoyote na wawakemee wale wanaotaka kupata madaraka kwa gharama yoyote.
Mbunge ajivua uanachama Chadema
Sumbawanga. Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi ametangaza kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akizungumza mjini Mpanda katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, jana Arfi
aliwaeleza wananchi wa Mpanda kuwa uanachama wake ndani ya Chadema
utakoma mara tu baada ya kuvunjwa Bunge Julai 9.
Ijumaa, 3 Julai 2015
Upinzani ‘walianzisha’ tena bungeni
Dodoma. Mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Ubungo
(Chadema), John Mnyika jana ulizua kizaazaa na kumlazimisha Spika Anne
Makinda kuahirisha kikao baada ya kukosekana utulivu ndani ya Ukumbi wa
Bunge.
Kikao hicho kiliahirishwa muda mfupi baada ya
kipindi cha maswali na majibu wakati Bunge lilipotakiwa kukaa kama
kamati kumalizia kiporo cha Muswada wa Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa
za Uhalifu na Mashahidi wa mwaka 2015 ambao mchakato wa kuupitisha
haukukamilika juzi kutokana na muda kuisha.
Alhamisi, 2 Julai 2015
Rick Ross ni jela au mtaani? Haya hapa kutoka Mahakamani na video yake..
Headlines za Entertainment Marekani zilikuwa na story ya Rick Ross kukamatwa na kuwekwa ndani yeye pamoja na bodyguard wake, kesi yao ilikuwa ni ishu ya kuteka na kujeruhi watu wawili.
July 01 2015 kapandishwa Mahakamani, Georgia Marekani.. Kesi ikasomwa na milango ikawa wazi kwa jamaa kuwekewa dhamanaWatuhumiwa wa EPA Waachiwa Huru.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru Kada wa CCM Rajabu Maranda na wenzake waliokuwa wanakabiliwa na kesi wizi wa Sh milioni 207 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Jopo la mahakimu watatu likiongozwa na Hakimu John Utamwa, Ignas
Kitusi na Eva Nkya liliwaachia washitakiwa hao baada ya upande wa
Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa hao.
Chadema yaibwaga ccm Mahakamani
Kiteto. Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya
Simanjiro mkoani Manyara imezidi kupata pigo baada ya Mahakama kutengua
matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji 16 vya mji mdogo wa
Mirerani, kwa maelezo kuwa ulikiuka sheria na utaratibu wa Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja
kwa Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo ambao uliwaweka
madarakani makada wa CCM.
LOWASA ACHOKA KUITWA FISADI
Dodoma. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana aliwataka wanaomhusisha na ufisadi kuacha mara moja kwa sababu hakuna hata chembe ya ukweli katika tuhuma hizo.
Lowassa, aliyeonekana kuzungumza kwa hisia,
alisema hayo jana mara baada ya kurejesha fomu ya kuwania kuteuliwa na
CCM kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Jumatano, 1 Julai 2015
WALIOMUUA ALBINO MWAKAJILA WA MBEYA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI
Hakimu Mwakalinga siku alipohukumiwa
kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Rungwe. Leo amehukumiwa tena kunyongwa mpaka kufa katika mauaji ya
mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya leo hii
imewahukumu kunyongwa mpaka kufa watu wanne kati ya watano waliomuua
Henry Mwakajila (17) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).
Waliohukumiwa kunyongwa mpaka kufa ni
Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga na Gerard Korosso
Kalonge (wakazi wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje), na Leonard
Msalage Mwakisole na Hakimu Mselem Mwakalinga (wakazi wa Kiwira wilayani
Rungwe).
Mshtakiwa wa nne, Mawazo Philemon
Figomole, ameachiliwa huru na mahakama hiyo baada ya ushahidi wa upande
wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasi na shaka kwamba alihusika katika
mauaji hayo.
Lowassa arejesha fomu za Uraisi, atoa onyo kali
Baada ya kukabidhi fomu hizo, Mh.
Lowassa, alikutana na waandishi wa habari na kusoma taarifa yake fupi,
ambapo alionya wale wote wanaoeneza habari potofu kuwa yeye ni mla
rusha, watoe ushahidi, wapi amekula rushwa, na ni kiasi gani, za nani
na wapi, Awataka Watanzania kupuuza habari hizo na kwani yeye ni
muadilifu na hana shaka na hilo.
MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2015 YATANGAZWA
Jumla ya wanafunzi 18,751 kati ya 73,754 (asilimia 74.58) waliofanya
mitihani ya kidato cha nne mwaka jana wamekosa nafasi za masomo za
kujiunga kidato cha tano na vyuo vya ufundi mwaka huu kutokana na sababu
mbalimbali.
Miongoni wa sababu hizo ni ufinyu wa nafasi za shule, kushindwa
kupata ufaulu wa masomo waliyochagua, umri mkubwa wa watahiniwa wa
kujitegemea pamoja na kukosa sifa za kuchaguliwa, huku muhula wa kwanza
wa kujiunga kidato cha tano ukitarajiwa kuanza Julai 18, mwaka huu.
Aidha, wanafunzi 479 wakiwamo wavulana 332 na wasichana 147
wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi mwaka huu, huku idadi ya
wanafunzi hao ikiongezeka kutoka 472 mwaka 2014 hadi 479 mwaka huu.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)