Keshi,53, ambaye aliteuliwa
tena kukinoa kikosi hicho mwezi April mwaka huu, ametimuliwa jana jioni,
huku msaidizi wake Salisu Yusuf pamoja na Kurugenzi ya Ufundi ya
Shirikisho hilo chini Amodu Shuaibu, wakishika nafasi hiyo mpaka maamuzi
mengine yatakapotangazwa.
“Baada ya kuipitia mara kadhaa
ripoti ya Kamati ya Nidhamu na kamati ya Ufundi na Maendeleo ya NFF,
lakini vilevile mwenendo na matendo ya Keshi kama kocha mkuu, tumegundua
kuwa kuna ukosefu wa dhamira ya dhati wa kufikia malengo ya Shirikisho
kama ilivyoainishwa katika makubaliano ndani ya mkataba,” ilisomeka
taarifa iliyotolewa na kamati ya utendaji ya NFF.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni