TANGAZO

TANGAZO

Jumanne, 10 Novemba 2015

CHALLENGE CUP: KILIMANJARO STARS YAPANGWA NA WENYEJI

John Bocco-Stars
Ratiba ya michuano ya Kombe la Challenji kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Senior Challenge Cup) imetoka jana ambapo timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imepangwa kundi moja na wenyeji Ethiopia.
Katika taarifa ya CECAFA iliyotolewa jana, Kilimanjaro Stars imepangwa kundi
A pamoja na wenyeji Ethiopia, Somali na waaalikwa wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’.
Kundi B lina  bingwa mtetezi timu ya Kenya, Uganda, Burundi na Djibouti, huku kundi C likiwa na timu za Rwanda, Sudan, Sudan Kusini na Zanzibar.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 nchini Ethiopia katika mji wa Addis Ababa na kumalizika Disemba 6 mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni