Ikiwa Ligi Kuu soka Tanzania bara imesimama kupisha mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Algeria na kupisha michuano ya Kombe la Challenge hadi December 12, homa ya dirisha dogo la usajili imeanza kwa vilabu kadhaa kuanza kuhusishwa kunyemelea saini za wachezaji.
Klabu ya Dar Es Salaam Young African ilikuwa inahusishwa kutaka kusajili wachezaji wawili mmoja wa kigeni ambaye anatajwa kuja kuchukua nafasi yam brazil Andry Coutinho huku wakihusishwa kumsajili kimya kimya beki wa Simba Hassan Kessy, Amplifaya ya Clouds FM imefanya exclusive interview na katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha ana majibu haya.
”
Nikwambie tu ukweli sisi tuna kikosi chetu ambacho tumekisajili toka
mwanzo wa msimu kwa ajili ya mashindano tofauti tofauti ila bado
sijapokea ripoti ya mwalimu akitaka kusajili, Andry Coutinho yupo na
bado ana mkataba na Yanga wa miezi 8, kuendelea nae inawezekana kama
mwalimu akimuhitaji, Kessy ni mchezaji mzuri na tungependa kuwa naye
lakini hadi sasa ni mchezaji wa Simba wala hayupo katika mipango yetu”
>>> Jonas Tiboroha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni