TANGAZO

TANGAZO

Jumatano, 11 Novemba 2015

TOTO AFRICANS YAITISHA MKUTANO WA DHARURA

Toto logo 

Mkutano Mkuu wa Dharula wa Klabu ya Toto Africans unatarajiwa kufanyika tarehe 22 Novemba Mwaka huu jijini Mwanza.
Taarifa hiyo imetolewa leo na mwenyekiti wa klabu hiyo Bw. Godwin Aiko wakati akizungumza na mwanamichezo wetu wa jijini Mwanza.

“Napenda kuwatangazia wanachama wote wa Toto Africans kuwa, mkutano wa dharura utafanyika siku ya Jumapili tahehe 22 November, 2015 jijini Mwanza”, amesema Aiko.
“Ni kawaida mkutano mkuu kufanyika mara moja kwa mwaka lakini kwasababu tulikuwa na mkutano wa kujaza nafasi za uongozi, katika mkutano huo tuliazimia kwamba mkutano mkuu wa dharura ufanyike kwa ajili ya kupata taarifa zote za fedha na shughuli za klabu mwaka 2014 na mwaka huu ambao tunaendelea nao”.
“Ajenda kuu itakuwa ni kupata taarifa ya maendeleo ya klabu kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na mipango ambayo tunayo ya kuendeleza klabu siku za mbele”.
“Ni kweli tunatatizo la ukata nafikiri nalo ni moja kati ya vitu vinavyofanya tukutane ili tuweze kuweka mipango thabiti kwa ajili ya kupata fedha za kutosha kwa ajili ya klabu”.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni