TANGAZO

TANGAZO

Alhamisi, 19 Novemba 2015

Hii ni Top 10 ya wachezaji wabunifu zaidi katika Ligi Kuu Uingereza na adui wa Taifa Stars ndani …



November 18 nimekutana na list ya wachezaji wabunifu zaidi katika Ligi Kuu Uingereza ila Top 10 hii iliyoandikwa na mtandao wa teamtalk.com imetaja majina ya wachezaji 10
yanayotajwa kuwa na ubunifu uwanjani kutokana na uwezo wao wa kutoa pasi za mwisho katika ufungaji wa magoli. List hii inaongozwa na kiungo wa kimataifa wa Ujerumani anayekipiga katika klabu ya Arsenal Mesut Ozil.
1- Mesut Ozil ana rekodi ya kuwa mchezaji anayeongoza kwa kutoa pasi za mwisho kwa Cristiano Ronaldo na kufunga wakati yupo Real Madrid. Ozil anatajwa kuwa na rekodi ya kutoa pasi za mwisho (assist) 10 katika mechi 11. Kwa ujumla Ozil anatajwa kutengeneza nafasi za magoli 54 ambapo ni wastani wa 4.9 kwa mechi moja.

during the Barclays Premier League match between XXX and XXX at Liberty Stadium on October 31, 2015 in Swansea, Wales.

                             Mesut Ozil

 2- Dimitri Payet anakipiga katika klabu ya West Ham United anatajwa kuwa na assist tatu tu nyuma ya Ozil ila Dimitri Payet anatajwa kutengeneza wastani wa nafasi 3.9 kwa mechi moja, hii inamuweka katika list hii

Payet-597027

    
Dimitri Payet
3- Christian Eriksen uwezo wa Eric Dier ana Dele Alli umekuwa ukionekana sana uwanjani kutokana na mchango wa Christian Eriksen , Eriksen anatajwa kuwa na rekodi ya kutengeneza wastani wa nafasi 3.1 kwa mechi.

ChristianEriksenapplauds_3213228 

4- Dusan Tadic ana rekodi nzuri pia na yakuvutia anatajwa kupiga wastani wa pasi 26.5 kwa mechi lakini pia amemudu kutengeneza jumla ya nafasi tatu kwa mchezo mmoja.
Southampton-vs-Norwich 

Dusan Tadic wa Southampton
5-  Kevin De Bruyne ana miezi michache toka arudi katika Ligi Kuu Uingereza kwa mara nyingine tena ila anaonekana kufanya vizuri katika Top 10 anatajwa kuwa na assist nne katika mechi saba alizoanza na moja akitokea benchi huyu ana wastani wa 3.0 ya utengenezaji wa nafasi za magoli uwanjani.
2BCF932900000578-0-image-m-3_1441275864832 
Kevin De Bruyne wa Man City
6- Santi Cazorla anacheza pamoja na Francis Coquelin katika kikosi cha Arsenal, ametengeneza wastani wa nafasi 2.9 katika mechi 12 na assist 3, lakini pia anatajwa kuwa na ratio ya 90.6% ya kupiga pasi zilizokamilika yaani bila kuharibiwa na adui.

maxresdefault

Santi Cazorla
7- Eden Hazard wachezaji wengi wa Chelsea msimu huu wanatajwa kufanya vibaya uwanjani ispokuwa Eden Hazard anaonekana kuendelea kufanya vizuri uwanjani na bado yupo nafasi ya saba kwa kutengeneza nafasi za magoli kwa kuwa na wastani wa 2.7.
LONDON, ENGLAND - FEBRUARY 08: Eden Hazard of Chelsea celebrates scoring during the Barclays Premier League match between Cheslea and Newcastle United at Stamford Bridge on February 8, 2014 in London, England. (Photo by Mike Hewitt/Getty Images) 
Eden Hazard
8- James Milner katika nafasi ya nane ametengeneza wastani wa nafasi 2.5 kwa mechi lakini anatajwa kuwa na assist tatu, hata hivyo ujio wa Jurgen Klopp unatajwa kumfanya mchezaji huyo kuongeza wastani wake wa kufanya vizuri uwanjani.
James Milner, Manchester City 
James Milner
9- Erik Lamela anatajwa kutengeneza wastani wa nafasi 2.4 hadi sasa na anatajwa kuanza jumla ya mechi nane na kufanya assist 3. Lakini ameingia mechi tatu akitokea benchi nje ya mechi nane alizoanza.
Erik-Lamela_3047709 
Erik Lamela wa Tottenham Hotspurs
10- Riyad Mahrez huyu anafunga Top 10 ya wachezaji wabunifu katika Ligi Kuu Uingereza lakini ni miongoni mwa wachezaji wa Algeria walioifunga Taifa Stars magoli 7-0, Riyad Mahrez akipachika goli la tatu dakika ya 43. Riyad Mahrez pia amefungana na Moussa Sissoko na Nathan Redmond katika Top 10 kwani wote wanawastani wa 2.2 kwa mechi





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni